Tunaendelea na uchambuzi wa timu za Kundi A katika michuano ya kombe la Shirikisho Afrika (CAF Conferation). Baada ya hapo awali kuichambua MO Bejaia, waarabu kutoka Algeria, leo tunaingazia timu ya Medeama SC.
Ikumbukwe tu kwamba, Yanga ipo kundi A pamoja na timu za TP Mazembe ya DRC, MO Bejaia ya Algeria na Medeama ya Ghana.
Medeama Sporting Club (Medeana SC). Hii ni timu inayopatikana katika eneo la Tarkwa linalopatika magharibi mwa Ghana. Ni timu inayoshiriki Ligi Kuu nchini humo (Glo Premier League).
Medeama ilianzishwa mwaka 2002, wakati huo ikijulikana kwa jina la Kessben F.C na kubadilishwa kuwa Medeama Sporting Club January 2011.
Katika michezo yake ya nyumbani, Medeana inatumia uwanja wa Abrankese uliopo jijini Kumasi huko Ashanti
Uwanja wa Abrankese ulianza kutumika mwaka 2007. Ni uwanja kwa ajili ya michezo mbalimbali lakini mara nyingi hutumika kwa mchezo wa soka. Uwanja huo una uwezo wa kuingiza watu 12,000.
Kabla ya kutumia uwanja wa Abrankese, Medeama walikuwa wakitumia uwanja wa Anane Boateng ambao waliutumia mpaka mwaka 2008.
Mdhamini Mkuu wa Medeama SC ni kampuni ya vinywaji baridi ya Coca Cola
Medeama hawana hata mchezaji mmoja katika timu ya taifa ya Ghana.
Wachezaji wote wanaounda kikosi timu hiyo ni raia wa Ghana. Ipo chini ya kocha Msweden Tom Strand.
Kuingia katika hatua ya makundi, Medeama ilitoa Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini kwa faida ya goli ugenini. Mchezo wa kwanza walifungwa 3-1 nchini Afrika Kusini na marudiano wakashinda 2-0, hivyo kuwa na wastani wa magoli 3-3.
Medeama kwa sasa wanashika nafasi ya 6 ikiwa na alama 23 nyuma ya alama 5 dhidi ya vinara Wa All Stars yenye alama 28.
Wana rekodi nzuri sana wanapocheza katika uwanja wao wa nyumbani, kwasababu katika michezo yao mitano ya mwisho, mitatu wamecheza nyumbani na yote wameshinda.
Ni timu yenye future kubwa kutokana na idadi kubwa ya wachezaji katika kikosi chao kuwa vijana. Hakuna mchezaji aliyezidi miaka 25.
Mshambuliaji wao wa kuchungwa zaidi ni Mohammed Abbas ambaye ndiyo amekuwa mwiba mchungu katika timu nyingi zilizocheza na Medeama
Rekodi yao katika michezi mitano ya mwisho
Historia yao katika vikombe.
Ghana Premier League: 0
FA Cup: 2, wamechukua mwaka 2013, 2015.
Ghana Super Cup: 1, wamechukua mwaka 2015.
SWAG Cup: 0
Annual Republic Day Cup: 0
Kikosi chao
0 comments:
Post a Comment