Friday, June 10, 2016

Michuano ya 15 ya Euro inaanza leo nchini Ufaransa huku kwa mara ya kwanza timu 24 zikitaraji kuchuana vikali kuwania taji hilo. 
Ufaransa, Uhispania, Ujerumani, Ubelgiji na England ndizo timu zinazopewa nafasi kubwa na kubeba ndoo hiyo mwaka huu.
Leo kutakuwa na mchezo mmoja tu wa ufunguzi ambapo wenyeji Ufaransa watakuwa wakipambana na Romani, mchezo wa kundi A utakaopigwa kunako dimba la Stade de France saa nne usiku (kwa saa za Afrika Mashariki). Timu nyingine katika kundi hilo ni Albania na Uswizi.
Tangu kuanzishwa kwa michuano hiyo mwaka 1927, wachezaji mbalimbali waliowahi kuwa na majina makubwa kutoka nchi mbalimbali wameacha alama zao katika historia ya michuano hiyo. Lakini hapa tunawaangazia wachezaji 15 tu wenye magoli mengi zaidi katika michuano hiyo.

15. ZINEDINE ZIDANE.
Huyu ni mfaransa ambaye alicheza kwa mafanikio makubwa katika ngazi ya klabu na timu ya taifa. Zidane amecheza Euro katika miaka ya 1996, 2000 na 2004. Alifanikiwa kucheza michezo 14 na kufunga magoli 5 tu.

13. FERNANDO TORRES 
Torres ni moja ya washambuliaji waliocheza kwa mafanikio makubwa katika timu yake ya taifa. Amecheza miaka ya 2004, 2008 na 2012. Amefanikiwa kucheza michezo 13 na kuweka kimiani magoli 5.

13. JURGEN KLINSMANN 
Huyu ni Mjerumani aliyekuwemo kwenye michuano hiyo katika taifa lake kwenye miaka ya 1988, 1992 na  1996. Alifanikiwa kucheza michezo 13 na kupachika mabao 5.

12. Milan Baroš
Mshambulizi huyu wa zamani wa Jamhuri ya Cech alifanikiwa kushiriki Euro na timu yake katika miaka ya 2004, 2008 na 2012. Katika miaka yote hiyo alifanikiwa kucheza michezo 11 na kufunga magoli 5.

11. MARCO VAN BASTEN 
Nguli huyu wa uholanzi alicheza michuano hiyo miaka ya 1988 na 1992. Alicheza michezo tisa na kuweka kambani magoli matano.

10. WAYNE ROONEY 
Anashikilia rekodi ya ufungaji bora wa muda wote England. Rooney amecheza michuano ya Euro mwaka 2004, 2012 na mwaka huu pia atakuwepo. Katika awamu mbili zilizopita, amecheza michezo 6 na kufunga magoli matano. Bado yupo katika kinyang'anyiro na pengine ataendelea kufunga mengi zaidi.

9. SAVO MILOSEVIC
Mshambulizi huyo wa zamani wa Yugoslavia alicheza mwaka 2000 tu. Alicheza michezo minne na kufunga magoli matano.

7. NUNO GOMES 
Nuno Gomez ni nyota wa zamani wa Ureno aliyecheza kwa mafanikio makubwa. Alicheza miaka ya 2000, 2004 na 2008. Alifanikiwa kucheza michezo 14 na kufunga magoli 6.

7. CRISTIANO RONALDO.
Huyu ni moja ya wachezaji hodari duniani kwa sasa. Ndiye nahodha wa Ureno kwa wakati huu. Amecheza miaka ya 2004, 2008, 2012 na mwaka huu pia atakuwepo. Amefanikiwa kucheza michezo 14 (ukiachana na mwaka huu ambapo bado hajacheza) na kufunga magoli 6.

6. THIERRY HENRY 
Mshambuliaji huyu wa zamani wa Ufaransa alishiriki michuano hiyo miaka ya 2000, 2004 na 2008. Alifanikiwa kucheza mechi 11 na kuweka kambani magoli 6.

5. ZLATAN IBRAHIMOVIC 
Huyu ni nahodha wa Sweden kwa sasa. Ameshiriki michuano hii katika miaka ya 2004, 2008, 2012 na mwaka huu pia yupo. Kabla ya michuano hii ya sasa, amecheza michezo 10 na kufunga magoli 6. Bado ana nafasi ya kujiongezea idadi ya magoli kutokana na uwepo wake katika michuano ya mwaka huu.

4. PATRICK KLUIVERT 
Ni moja ya washambuaji bora wa Uholanzi kuwahi kutokea. Ameshiriki kwenye michuano hiyo katika miaka ya 1996 na 2000. Alicheza michezo 9 na kufunga magoli sita.

3. RUUD VAN NISTELROOY 
Mdachi huyu alikuwa mwiba mchungu kwa safu za ulinzi za timu pinzani. Alishiriki na uholanzi kwenye michuano ya Euro katika miaka ya 2004 na 2008. Alicheza michezo 8 na kufunga magoli 6.

2. ALAN SHEARER 
Shearer ni moja ya washambuliaji bora waliowahi kutokea katika taifa la England. katika maisha yake yote ya soka ameshiriki michuano ya Euro miaka ya 1992, 1996 na 2000. Alifanikiwa kufunga magoli 7 katika michezo 9.

1. MICHEL PLATINI 
Licha ya kucheza miaka mingi iliyopita, Platin ambaye ni mfaransa bado anashikilia rekodi ya kufunga magoli mengi zaidi. Alicheza michuano hiyo mara moja tu, ambapo ilikuwa ni mwaka 1984 na kufunga magoli 9 ndani ya michezo 5.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video