Friday, June 10, 2016

KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, imezidi kujitanua kimasoko na kuwafikia zaidi mashabiki wa soka nchini baada ya asubuhi hii kuzindua uuzwaji wa vifaa vyake vya michezo kwenye boti zinazokwenda Unguja, Zanzibar.

Hii itakuwa ni mara ya pili kwa Azam FC inayodhaminiwa na Benki ya NMB kuendeleza mradi wa uuzwaji bidhaa zake baada ya Mei 24 mwaka huu kuzindua duka kubwa la kuuza vifaa vyake vya michezo lililopo Mtaa wa Mkunguni na Swahili, Kariakoo, jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya vifaa hivyo ni pamoja na jezi, fulana, ‘track suit’, makoti ya mvua, kofia, soksi, raba za mazoezi, taulo, mipira, bendera, mabegi ya mgongoni na kusukuma, kalamu, vyote vikiwa na nembo ya klabu hiyo ambao ni mabingwa watetezi wa michuano mikubwa ya Afrika Mashariki na Kati ngazi ya vilabu (CECAFA Kagame Cup).  

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa aina hiyo nyingine ya uuzaji wa vifaa vyake leo ndani ya boti ya Azam Kilimanjaro (vi) , Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba, alisema kuwa lengo kuu la kuuza jezi kwenye boti ni kuzidi kuwafikia mashabiki wa timu hiyo na Watanzania kwa ujumla pamoja na kuongeza namba yao.

“Kwanza tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwamba dhamira yetu inazidi kuendelea na kuwafikia Watanzania na tunashukuru Wakurugenzi wote wa bodi nzima ya timu kwa sababu bila ya wao tusingeweza kufika hapa, Azam FC lengo letu ni kuwafikia wadau wengi wa mpira kwa sababu ndio washangiliaji wetu na wanatakiwa wawe kwenye sare zetu kila wanapokuja kutushangilia,” alisema.

Biashara yazidi kupaa

“Kama mnakumbuka mwezi uliopita, tulizindua duka letu Kariakoo na tayari watu wengi wameweza kufika pale, lakini bado mahitaji yamekuwa ni makubwa na hatuwezi kumfikia kila mtu, baada ya kuona hivyo tukawaomba Wakurugenzi wa bodi kuongeza jambo hili jingine ili kuwafikia na kuwasaidia Watanzania wengine wanaofanya safari zao kila siku za kwenda Unguja, na wakubwa wenyewe wametukubalia,” alisema.

Kawemba alisema baada ya uzinduzi huo,vifaa vyote vya klabu hiyo vitakuwa vikipatikana kwenye boti zote zinazokwenda Unguja, huku pia hivi karibuni wakitarajia kuzindua duka jingine la vifaa katika eneo la feri ili kuendelea kurahisisha zaidi upatikanaji wa bidhaa zao.

“Kama mnavyoona vifaa vinavyouza kwenye boti hii, tutakuwa tukifanya hivi kwenye boti zote zinazokwenda Unguja kuanzia leo ambapo kutakuwa na bidhaa zote za Azam FC ambazo kila mtu atazipata pale atakapokuwa anazihitaji, lakini kubwa zaidi hivi karibuni tutafungua duka letu feri pale wanapouzia tiketi za boti, kwa hiyo hilo litawasaidia wasafiri wote kununua vifaa vya klabu yetu, akikosa kununua wanapouzia tiketi basi atavipata ndani ya boti,” alisema.

Kusudio kuu la mradi huo

Bosi huyo alisema dhamira yao ni ile ile ya kuhakikisha wanawafikia Watanzania wengi zaidi na kuongeza idadi ya namba ya mashabiki wa timu hiyo.

“Tunataka kuwafikia watu wengi kwa haraka zaidi ni kipindi cha kujiandaa na msimu mpya sasa (pre season), tunajiandaa kuhakikisha tunapata watu wengi watakaoweza kuikubali klabu yetu na tunaamini kabisa watu wapo kwa kuwa wamekuwa wakiulizia na kuhitaji bidhaa zetu,” alisema.

Kwa nini Unguja?

“Watu watajiuliza sana kwa nini Unguja, Azam FC tunaasili kubwa na Unguja, kwa hiyo tunakwenda nyumbani, na tunawathamini mashabiki wengine wetu popote pale walipo na kadiri timu itakapokuwa insafiri kwenda kucheza mechi za Ligi Kuu, tutakuwa tunachukua bidhaa zetu na kwenda nazo.

“Kwa hiyo kwa washabiki wengine waliopo sehemu nyingine Tanzania wasijisikie wanyonge na kusema kwanini Azam FC inakwenda Unguja peke yake, kama nilivyosema tuna historia kubwa na Unguja na pia tuna historia na sehemu nyingine kwa kuwa wachezaji wetu wanatoka sehemu tofauti tofauti nchini,” alisema.

Kuhamia viwanja vya ndege

Katika kutanua zaidi masoko yake na kuwafikia mashabiki, Ofisa huyo alisema kuwa kwa hapo baadaye pia wanatarajia kuuza bidhaa hizo kwenye viwanja vya ndege nchini.

Atoa wito kwa Watanzania

Aliongeza kuwa: “Vifaa vyote hivyo tumeviweka nembo yetu ili kuitunza, ni vizuri watu wakaheshimu hivyo tunajua wengine wataingia kati na kuuza bidhaa zetu zisizo halisi (feki), tunawaomba watu wote wanapohitaji vifaa vyetu halisi vya Azam FC vyenye ubora ule ule wanavyotumia wachezaji wetu, watavipata kwenye maeneo hayo, jezi zikiwa ni shilingi 15,000 tu,” alisema.

Mkuu wa vioski afurahia

Naye Mkuu wa maduka yote (vioski) ndani ya boti za kisasa za Azam, Salum Ahmed, hakusita kuelezea furaha yake kupitia mtandao wa klabu www.azamfc.co.tz,  huku akidai kuwa watu wengi wamekuwa wakiulizia bidhaa hizo kabla ya kuzinduliwa.

“Nimefurahia sana kwani hili suala limekuja kwenye muda muafaka, watu wengi wamekuwa wakituuliza mara kwa mara wakihitaji vifaa vya Azam FC na tumekuwa tukiwaelekeza waende Kariakoo, hivyo bidhaa hizo kuanza kuuzwa hapa ni jambo zuri naamini tutakuwa tumekata kiu yao, napenda kuwaambia wote wanaokuja kupanda boti zetu hivi sasa hawatapata usumbufu wa awali kwani bidhaa zote watazipata humu,” alimalizia mkuu huyo.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video