Utafanyaje ikitokea una watoto wawili ambao wote umewazaa mwenyewe lakini wanacheza kwenye mataifa tofauti, je, siku rimu zao zikikutana utamsapoti nani....mmoja au wote?.
Sasa ona hapa alichofanya mama wa Granit Xhaka na Taulant Xhaka jana katika mchezo wa jana wa Euro kati ya Uswizi na Albania mabapo Uswizi walishinda bao 1-0. Katika mchezo huo Granit alikuwa akichezea Uswizi wakati Tualant alikuwa upande wa Albania.
Mama yao Granit na Taulant akionesha mahaba kwa watoto wake wote. |
Licha ya wote wawili kuzaiwa Uswizi lakini wawili hao waliamua kuchagua kucheza mataifa tofauti. Asili ya wazazi wao ni kutoka Kosovo huko Albania.
Lakini mama ni mama tu, jana mama yao Granit na Taulant akishuhudia mtanganange baina ya watoto wake, aliamua kutafuta namna ya kujigawa ili awasapoti vijana wake wote. Aliamua kuvaa tisheti ambayo nusu ina rangi ya bendera ya Albania na nusu rangi ya bendera ya Uswizi.
Hiyo ilikuwa maalum kwa ajili ya kuonesha upendo kwa watoto wake wote bila ya kubagua.
Hivi karibuni Granit alisajiliwa na Arsenal kwa ada ya oaundi milioni 35
Katika mchezo wa jana Granit ndiye mchezaji aliyegusa mpira mara nyingi zaidi kuliko wote uwanjani.
Wawili hao ambao walikulia katika academy ya Basel wanakuwa wa kwanza katika historia ya kucheza mataifa mawili tofauti katika michuano ya Ulaya.
0 comments:
Post a Comment