Mlinzi wa Villarreal Eric Bailly amefuzu vipimo vya afya tayari kwa ajili ya kujiunga na Manchester United.
United walikuwa wakipata upinzani mkubwa kuwania saini ya beki huyo Muivory Coast kutoka kwa mahasimu wao Manchester City, Barcelona na Paris Saint Germain, lakini wameonekana kuwa na mkono mrefu zaidi na kushinda mbio hizo.
Kufuatia utitiri wa vilabu mbalimbali katika kuwania saini ya beki huyo, gharama za usajili wake zimepanda na kufikia paundi milioni 30. Msimu uliopita Bailly ameicheza Villareal michezo 25 na kuonesha kiwango cha kuridhisha.
He joined Villarreal from Espanyol in January 2015 for a fee of around £5m as a replacement for Gabriel Paulista, who had moved to Arsenal earlier that month.
Alijiunga na Villareal akitokea Espanyol mwaka 2015 kwa ada ya paundi milioni 5 akirithi mikoba ya Gabriel Paulista ambaye alijiunga na Washika Bunduki wa London Arsenal.
Mpaka sasa Bailly amecheza mara 14 kwenye timu yake ya taifa na alikuwa miongoni mwa wachezaji walifanikisha kutwaa taji la Afrika mwaka 2015, huku akifanikiwa kufunga mkwaju wa penati katika mchezo wa fainali dhidi ya Ghana.
0 comments:
Post a Comment