Saturday, June 11, 2016

Payet
Bao la dakika za lala salama limewapa ushindi Ufaransa dhidi ya Romania kwenye mchezo wa ufunguzi wa michuano ya Euro 2016 kwenye uwanja wa Stade de France.

Ulikuwa ni usiku wa kukumbukwa na wananchi wa Ufaransa kutokana na mashabiki karibu 130 kupoteza maisha kwenye uwanja huo mwezi November mwaka jana baada ya kulipuliwa na bomu, Payet aliihakikishia ushindi timu yake kwa mkwaju mkali akiwa umbali wa takribani mita 30 toka lilipo goli.
Ufaransa ambao walifanikiwa kunyakuwa mataji mawili makubwa yaliyofanyika kwenye ardhi ya kwao, mwaka 1984 walibeba ndoo ya Euro na mwaka 1998 wakachukua kombe la dunia wanatajwa kuwa miongoni mwa timu ambazo zinapewa nafasi ya kunyakua kombe la Euro mwaka huu.

Lakini baada ya mpira wa kichwa wa Antoine Griezmann kugonga mwamba, kikosi cha Ufaransa kilihangaika kupata bao mbele ya Romania ambao pia walitengeneza nafasi nzuri kadhaa za kufunga.

Ufaransa inapata ushindi kwenye mchezo wake wa ufunguzi

Kikosi cha Les Bleus ilibidi kisubiri hadi dakika ya 58 kupata bao la kwanza, ambapo Olivier Giroud aliunganisha kwa kichwa krosi ya Payet na kuiandikia timu yake bao la kuongoza.
Romania walijibu mapigo ndani ya dakika saba tu, Bogdan Stancu akifunga kwa mkwaju wa penati baada ya Patrice Evra kumfanyia madhambi Nicolae Stanciu kwenye eneo la hatari.
Mchezo huo ulianza kutazamwa kuwa utamalizika kwa sare hadi pale Payet alipofanya kazi ya ziada kuifungia bao la ushindi timu yake dakika ya 89 kwa juhudi zake binafsi, matokeo ambayo yalikuwa yakisubiriwa na kila mfaransa.
Star huyo wa West Ham licha ya kufunga bao la ushindi, kiwango kilichooneshwa na timu ya Ufaransa hakikuwa cha kuvutia lakini matokeo ya ushindi yalikuwa ni muhimu kwenye mchezo huo.
Ushindi kwenye mchezo huo ulikuwa ni muhimu kwa Ufaransa hasa ukizingatia wao ndiyo wenyeji wa michuano, inaaminika itasaidia kuwafanya wafaransa kuwa kitu kimoja kama nchi katika kipindi hiki cha mashindanbo baada ya kuwepo na migomo na maandamano ya wanachi.
Ulinzi ulikuwa umeimarishwa kwa kiasi kikubwa nje ya uwanja wa Stade de France, kukiwa na sehemu mbili tofauti za kufanyiwa ugaguzi kwa mashabiki ambao walikuwa wanaingia uwanjani hali iliyopelekea mchezo kumalizika salama bila tukio lolote lililohatarisha usalama.

Payet adhihirisha kuwa yeye ni star

Paul Pogba ndiey alitarajiwa kuwa star wa timu ya Ufaransa, lakini alikuwa ni Payet ambaye alionesha kiwango cha juu kwenye mchezo dhidi ya Romania.

Mchezo huu utakumbukwa kutokana na goli lake la ushindi lakini pia alikuwa nyuma ya kila shambulizi lililotengenezwa na Ufaransa.

Kabla hajapika bao la Giroud, alimtengenezea nafasi striker huyo wa Arsenal pamoja na Griezmann lakini wote walizipoteza nafasi hizo.

Sifa pia ziwaendee Romania ambao wamethibitisha kwanini wamekuwa na safu nzuri ya ulinzi katika mechi za kufuzu lakini pia wachezaji wa Ufaransa hawakuwa kwenye kiwango kilichotarajiwa na wengi.

Mpira wa volley uliopigwa na Pogba uliokolewa kwa ustadi na Ciprian Tatarusanu.

Man of the match-Dimitri Payet (Ufaransa)
Kocha wa Ufaransa Didier Deschamps siku za hivi karibuni alisikika akisema “kila mara anapogusa mpira, kuna jambo linatokea” na nyota huyo wa West Ham amethibitisha hilo.

Alikuwa nyuma ya kila tukio zuri la Les Bleus na kuonekana na ndiye mchezaji pekee aliyeweza kuwafungua Romania.

Dondoo muhimu
  • Romania hawajawahi kushinda mechi ya ufunguzi ya michuano ya Ulaya wametoka droo mara tatu na kupoteza mara mbili (D3 L2).
  • Olivier Giroud sasa amefunga magoli 8 kwenye michezo yake 6 ya mwisho aliyoanza kwenye kikosi cha Ufaransa.
  • Hadi sasa zimetoka penati tatu kwenye mechi za ufunguzi za michuano ya Euro kwenye misimu minne iliyopita ya mechi za ufunguzi (2004, 2012 na 2016), zote zikitokea dhidi ya timu wenyeji.
  • Kingsley Coman amekuwa mchezaji mdogo zaidi kuichezea Ufaransa kwenye michuano mikubwa ya kimataifa (akiwa na miaka 19 na siku 362).


0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video