Sunday, June 19, 2016

▪UHALALI WA KLABU KUMTUMIA MCHEZAJI WAKE MPYA CAF
"Suala la kama hakuna malalamiko katika klabu anayotokea ni muhimu sana, baada ya hapo ni kuangalia kama usajili wa michuano hiyo umefuatwa. Kuna aina mbili, kwenye mtandao na kawaida.
“Kama Caf imetoa leseni, kunakuwa hakuna shida. Lakini kunaweza kuwa na angalizo la kuangalia kama mchezaji hana mkataba tena na klabu aliyotokea au walimalizana kwa kufuata taratibu zote.
“Kama atakuwa amemaliza mkataba na klabu aliyotokea, hakika hakuna tatizo hata kidogo na linaloangaliwa hapo ni hivi; usajili wa Caf umekamilika? Leseni imetoka? Kama hayo yametekelezwa, hakuna tatizo,”

▪ SUALA LA HASSAN KESSY RAMADHANI NA WENGINE WAPYA
Msemaji wa CAF Junior Binyam amefafanua: 
“Nimeambiwa Yanga wamezungumza na wenzetu wakati wa pre-match meeting kule Algeria, wameuliza maswali yote na kujibiwa vizuri na wameelewa.
“Ninaamini wachezaji wao watakuwa hawana tatizo kwa maana ya usajili wa CAF. Kwenye suala la usajili katika klabu walizotoka, hili tunaweza kusubiri chama cha nchi yenu (TFF) ndiyo waseme. Lakini hadi sasa, inaonekana wachezaji hao wanaweza kutumika, hilo tuwaachie wao (Yanga).”

▪HITIMISHO.
Kwa kauli hiyo inaonekana Yanga, wana kila sababu ya kuwatumia Kessy, Juma Mahadhi, Andrew Vicent ‘Dante’ na Beno Kakolanya ambao wamesajiliwa. Sio mpaka Simba SC ama vilabu vingine wathibitishe hata TFF wanaweza fanya hivyo, hata bila ya uthibitisho kutoka upande wowote Yanga wanaweza kuwatumia ila kinachoonekana ni CAF walitoa tu angalizo kuwa Yanga wahakikishe wanawatumia wachezaji ambao wamekamilisha sajili pia wachezaji hao wawe hawana pingamizi zozote kutoka vilabu vyao walivyotoka, lakini Obrey Chirwa raia wa Zambia atalazimika kusubiri wakati Yanga ikipambana kumtafutia usajili wake wa leseni kutoka Caf.
Credit: Naipenda Yanga.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video