Dunia nzima imeguswa na kifo cha bondia bora kabisa kuwahi kutokea duniani wa uzito wa juu Muhammad Ali, baada ya kukutwa na umauti jana katika hospitali ya Phoenix iliyopo Arizona, Marekani. Ali alikuwa akisumbuliwa na matatizo katika mfumo wake wa upumuaji.
Kifo chake kimegusa watu mbalimbali maarufu ulimwenguni akiwemo rais wa Marekani Barack ambaye amesema kwamba Ali “aliushtua ulimwengu” wakati huo huo akisitiza kwamba ulimwengu umenufaika na mchango mkubwa wa bondia huyo enzi za uhai wake.
Mastaa wa soka hasa wa Afrika, pia hawakuwa nyuma katika kutoa rambirambi zao kwa bingwa huyo wa zamani wa wa ngumi za uzito juu mara tatu ambaye alijulikana kama 'The Greatest of All'.
Hizi ni baadhi ya tweet kutoka kwa mastaa wa soka wa Afrika.
0 comments:
Post a Comment