Arsenal wanazungumza na Leicester kukamilisha usajili wa winga Riyad Mahrez, 25, baada ya kukamilisha uhamisho wa Jamie Vardy, 29 (Sun), Arsenal wana uhakika Vardy atasaini kabla hajakwenda Ufaransa kwenye michuano ya Euro 2016 (Telegraph), Vardy amepewa mshahara wa pauni 120,000 kwa wiki na Arsenal (Leicester Mercury), Leicester wanamnyatia mshambuliaji wa Watford Troy Deeney, 27, kuziba nafasi ya Vardy (Telegraph), Pep Guardiola anataka kuimarisha kikosi cha Man City kwa kumtaka Toni Kroos, 26, kutoka Real Madrid, huku Fernando, 28, akisakwa na Villareal na Valencia (Manchester Evening News), winga wa Chelsea Eden Hazard ametupilia mbali tetesi kuwa anataka kujiunga na PSG, akisema hana mipango hiyo (Telefoot), PSG wako tayari kumshawishi kiungo wa Leicester N'Golo Kante, 25, kwa mkataba wa miaka mitano (Daily Mirror), Everton watataka kumsajili beki wa Crystal Palace Scott Dann, 29, kwa pauni milioni 15, iwapo Ronald Koeman atakwenda Goodison Park kutoka Southampton (Liverpool Echo), kipa wa Manchester United David De Gea, 25, huenda akaendelea kuwepo Old Trafford baada ya Real Madrid kuamua kutotoa kitita cha kutengua ada ya uhamisho cha pauni milioni 39 kilichopo kwenye mkataba wake (AS), meneja mpya wa Man Utd Jose Mourinho amemchukua mreno mwenzake Ricardo Formosinho, 59, kuwa msaka vipaji vya kiufundi Old Trafford (The Sun), United wametoa dau la pauni milioni 35.2 kumtaka kiungo wa Valencia Andre Gomes, 22 (Daily Star), na hatimaye.. meneja mpya wa Man Utd Jose Mourinho amemkaribisha Pele katika "makazi yake mapya" baada ya kukutana naye kwenye mchezo wa hisani Old Trafford.
Credit:Salim Kikeke
Credit:Salim Kikeke
0 comments:
Post a Comment