Manchester United huenda wakalazimika kutoa pauni milioni 78 kumsajili kiungo wa Juventus Paul Pogba, 23, miaka minne baada ya mchezaji huyo kuondoka Old Trafford (Daily Mirror), Manchester City wameacha kumfuatilia Pogba ambaye Mourinho pia alijaribu kumsajili akiwa Chelsea (Guardian), Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa, 27, anataka kurejea Atletico Madrid msimu ujao kwa mujibu wa rais wa klabu hiyo ya Spain (Antena 3 Sports, via Metro), Antonio Conte anataka kufanya usajili wake wa kwanza Kama meneja wa Chelsea kwa kumchukua beki wa kulia wa Juventus Stephan Lichtsteiner, 32,(Sun), Kiungo wa Roma Radja Nainggolan, 28, amezungumza na Conte kuhusu kuhamia Chelsea na kusema wachezaji wenzake wa timu ya taifa ya Ubelgiji Eden Hazard na Thibaut Courtois wamemsihi ahamie Stamford Bridge. (Daily Telegraph)
Meneja wa Manchester City Pep Guardiola haruhusiwi kusajili mchezaji yeyote kutoka Bayern Munich, Hii ni kwa mujibu wa kiungo wa mabingwa hao wa Ujerumani Douglas Costa, 25. (Globo Esporte, via Manchester Evening News), Baada ya kumsajili Eric Bailly kutoka Villarreal, Manchester United wanataka kusajili beki mwingine (Manchester Evening News), Man Utd pia wanamtaka mshambuliaji wa Juventus Alvaro Morata, 23. (Marca)
Lakini United wako tayari kumruhusu Matteo Darmian kuondoka huku Juventus wakiwa na nafasi kubwa ya kumsajili beki huyo (Tuttosport, via Gazzetta dello Sport), Mshambuliaji wa Arsenal Theo Walcott, 27, hana mpango wowote wa kuondoka Emirates licha ya klabu hiyo kupanda dau la kumnunua Jamie Vardy kutoka Leicester (ESPN)
0 comments:
Post a Comment