Saturday, June 18, 2016

Manchester United, Paris St-Germain na Real Madrid wako tayari kulipa ili kuununua mkataba wa Neymar kutoka Barcelona. Mchezaji huyo 24, ataruhusiwa kuzungumza na klabu yoyote itakapokuwa tayari kulipa pauni milioni 157 (Manchester Evening News)
beki wa Man Utd Phil Jones, 24, ameambiwa na meneja wake mpya Jose Mourinho kuwa bado anahitajika Old Trafford na kuwa, anaweza kuwa kama John Terry alivyokuwa Chelsea. (Daily Mirror)
Winga wa Borussia Dortmund Henrikh Mkhitaryan, 27, anataka kuondoka Ujerumani na kwenda Manchester United, kwa mujibu wa wakala wake (Daily Mail)
Meneja mpya wa Everton Ronald Koeman anaamini ni muhimu kuwa na mkurugenzi wa michezo kufanya naye kazi (Liverpool Echo)
Meneja wa zamani wa Manchester City Manuel Pellegrini ni mmoja wa makocha wanaowania nafasi ya kiufundisha Southampton. Wengine ni Claude Puel na Vitor Pereira. (Daily Telegraph)
Beki wa Manchester City Pablo Zabaleta, 31, anakaribia kuondoka Etihad na yuko tayari kupokea dau kutoka kokote (Manchester Evening News)
Tottenham wamekubaliana ada ya pauni milioni 11 kumsajili kiungo wa Southampton Victor Wanyama, 24, na Mkenya huyo atafanya vipimo vya afya wiki ijayo (Daily Mirror)
Sunderland watamfuatilia mshambuliaji wa Wolfsburg Bas Dost, 27, iwapo mazungumzo ya kumsajili Diafra Sakho, 26, kutoka West Ham yatavunjika (Sunderland Echo)
Crystal Palace nao wanamtaka mshambuliaji wa West Brom Saido Berahino, 22, kwa pauni milioni 15m na watazungumza na wawakilishi wake wikendi hii (Daily Mirror)
Leicester, Everton na West Ham wanafikiria kumsajili Mshambuliaji wa AC Milan M'Baye Niang, 21. (Guardian)
West Brom hawataki tena kumsajili beki wa kushoto wa Lyon Henri Bedimo, 32, ambaye mkataba wake unaisha mwezi ujao (Birmingham Mail) Kiungo wa
Leicester N'Golo Kante, 25, amekataa tena kuzungumzia mkataba mpya na klabu yake huku kukiwa na tetesi kuwa Real Madrid wanamtaka (Leicester Mercury)
Makamu mwenyekiti wa Leicester Aiyawatt Srivaddhanaprabha ana uhakika Mshambuliaji Jamie Vardy, 29, atakataa kwenda Arsenal na kubakia King Power Stadium. (Daily Mail) Celta Vigo wanewaambia Manchester City kuwa wanaweza kumsajili winga wa Spain Nolito kwa pauni milioni 14. (Manchester Evening News)
Meneja wa Newcastle Rafa Benitez anataka kumsajili Reece Oxford kutoka West Ham. Mchezaji huyo 17, anafuatiliwa pia na Manchester United, Manchester City na Arsenal (The Sun)

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video