Wednesday, June 15, 2016

Beki wa Everton John Stones, 22, anasakwa na Manchester United na Manchester City (Daily Star), Manchester City wanatarajia kutangaza usajili wao wa pili ambao ni winga kutoka Schalke, Leroy Sane, 20 (Marca), wakala wa kiungo wa West Ham, Dimitri Payet amesema "fedha nyingi sana" zitahitajika kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Ufaransa (Sky Sports), meneja mpya wa Everton Ronald Koeman anataka kumsajili kipa wa Newcastle Tim Krul, na pia anafikiria kumchukua kiungo wa Zenit St Peterburg, Axel Witsel, 27 (Daily Express), Manchester United wanakaribia kumsajili Zlatan Ibrahimovic, huku maslahi binafsi yakiwa tayari yameafikiwa na vipimo vya afya kufanyika baada ya Euro 2016 (Sky Sports), hata hivyo Man Utd huenda wakapata ushindani kutoka Bayern Munich, ambayo meneja wake mpya Carlo Ancelotti aliwahi kuwa kocha wa Ibrahimovic akiwa Paris St Germain (Bild), Stoke City wameanza mazungumzo na West Brom kutaka kumsajili mshambuliaji Saido Berahino, 22 kwa pauni milioni 5 (Daily Mail), beki kutoka Ufaransa Aymeric Laporte ameamua kusalia Athletic Bilbao akisema ndio uamuzi bora kwa sasa. Mchezaji huyo, 22 alikuwa akinyatiwa na Manchester City (Tovuti ya Athletic Bilbao), kipa wa Arsenal Wojciech Szczesny, 26, ambaye amecheza kwa mkopo Roma baada ya kuwasili kwa Petr Cech Emirates, amesema atafanya uamuzi kuhusu hatma yake baada ya Euro 2016 (Daily Star), Diego Simeone ataendelea kusalia Atletico Madrid baada ya kusaini mkataba mpya (AS). 
Credit:Salim Kikeke.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video