Tuesday, June 21, 2016

Kikao cha Rais wa SSC Evans Aveva na Viongozi wa matawi ya SSC wilaya ya Kinondoni kilichofanyika Jumapili ya tar 19/06 pale kwenye ukumbi wa Ngawaiya,Manzese-Argentina,ambapo tawi la Simba Dume-Temboni liliwakilishwa na Mwenyekiti wake Ben SHIJA na mjumbe wa kamati ya utendaji ya tawi Josephat SHILOGILE, kwa kauli moja kiliazimia yafuatayo:-
1.Kutokuwa na imani na Makamu wa Rais wa SSC Geoffrey KABURU ambaye amekuwa akiihujumu timu yetu kwa kutoa siri zetu kwa wapinzani wetu hasa Yanga, vile vile kugawa na kujenga matabaka kwa wachezaji.
-Pia imethibitika kuwa ni mpenzi mkubwa wa YANGA kwani baadhi ya wanasimba aliosoma nao UDSM wamedai kuwa kuanzia mwaka 1991-1993 alikuwa ni Mwenyekiti wa Tawi la Yanga chuoni hapo huku Mh.James Mbatia akiwa mwenyekiti wa tawi SSC chuoni hapo.
-Kutuhujumu kwenye mechi yetu na Yanga pamoja na ile ya Toto baada ya kuhongwa pesa na matajiri wa Yanga.
2.Kutokuwa na imani na mjumbe wa Kamati ya utendaji wa kuchaguliwa Said Tully ambaye amekuwa akishirikiana na Kaburu kuhujumu timu,pamoja na kutumia nafasi yake ya ujumbe kwenye kamati ya usajili kutaka 10 percent kwa wachezaji wanaotaka kusajiliwa na hii alishafanya kwa Malimi Busungu na Deus Kaseke na hivi sasa amedai 10percent kwa Miraji Adam. 
3.Tumemuamuru Rais Aveva kwenye mkutano mkuu aje na majibu ya kutosha kuhusu uwekezaji kwenye klabu yetu hasa suala la MO na ujenzi wa uwanja ili kukabiliana na ukata kwenye  timu yetu.. Kwani mpira wa sasa duniani kote unaendeshwa kwa uwekezaji na ubia na makampuni au matajiri. 
3.Jipu la kampuni ya EAG nalo litumbuliwe kwani hatuoni kazi yake zaidi ya kututengenezea kadi zisizokuwa na viwango na hatuoni faida yake kwa klabu.. Hivyo tumemshauri Rais aunde kitengo cha masoko na mauzo cha klabu na aajiriwe meneja kusudi kampuni ya EAG ifanye kazi chini ya kitengo hicho. 
4.Siku ya mkutano mkuu tupate hesabu kamili ya jezi,T-shirt na bidhaa mbalimbali za SSC zilizouzwa na zimeingiza kiasi gani... 
Hivyo basi kazi kwenu wanachama kujitokeza kwa wingi siku ya mkutano mkuu  hapo tar 10/07na sote tutekeleze maazimio hayo kwa ustawi wa klabu yetu... Na mwisho kabisa sisi kama wilaya ya Kinondoni tumepitisha kauli mbiu yetu ya MIMI NI SIMBA,SIMBA NI YANGU kuelekea msimu ujao wa ligi kuu na FA Cup

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video