Thursday, June 16, 2016

Klabu ya Simba SC imekamilisha Usajili wa  kiungo mahiri wa Mtibwa Sugar, Mzamiru Yassin.
Mzamiru ameithibitishia MPENJA SPORTS kuwa tayari amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia timu hiyo kuanzia Msimu wa 2016/2017.
"Mambo yangu na Simba yapo vizuri, nimesaini mkataba wa miaka miwili". Alisema kwa ufupi Mzamiru.
Nyota huyo mwenye uwezo wa kupiga pasi za uhakika na za chini chini anaungana na viungo wengine waliopo Simba, Mwinyi Kazimoto, Jonas Mkude, Justice Majabvi na Said Ndemla.
Kuondoka kwa Mzamiru ni pigo lingine kwa Mtibwa kwani tayari mlinzi wa kati Andrew Vicent 'Dante' ameshasajiliwa na Yanga sc, huku zikiwepo ripoti kwamba Simba inawataka pia wachezaji wengine wa wakata miwa hao wa Manungu, Mohamed Ibrahim na Shiza Kichuya ambao wote wanaichezea timu ya Taifa ya soka ya Tanzania, Taifa Stars.
Huyu anakuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa na Simba baada ya Emmanuel Simwanza kutoka Mwadui na Jamal Simba Mnyate kutoka Mwadui.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video