Wednesday, June 8, 2016

Nigeria wamepata pigo baada ya taarifa kwamba Stephen Okechukwu Keshi aka 'the Boss' amekufa ghafla mapema leo asubuhi.
Mchezaji huyo wa zamani  ambaye pia mwaka jana alimpoteza mkewe Kate aliyeishi naye kwa miaka 33 kutokana na ugonjwa wa kansa, inaarifiwa amekufa kutokana na matatizo ya moyo huko Benin, Edo State.
Kwa mujibu wa wanafamilia na marafiki zake wa karibu, Keshi hakuonesha dalili zozote za kuumwa. Alikuwa akiishi na watoto wake wanne pamoja na mama yake mzazi.
Mwaka 2013 aliweka rekodi baada ya kuipa Nigeria kombe la Mataifa ya Afrika na kuwa kocha pekee mzawa kufanya hivyo. Pia anashilikilia rekodi ya kuwa kocha wa pili kushinda kombe hilo akiwa kama mchezaji na baadaye kocha.
Mtu mwingine aliyeweza kufanya hivyo ni Mahmoud El-Gohary wa Misri.
Aliiwakilisha Nigeria kuanzia mwaka 1982, akiwa na umri wa miaka 20, mpaka mwaka 1994, mara nyingi aliitumikia Nigeria kama nahodha na kufunga magoli muhimu hasa ukizingatia nafasi yake aliyokuwa akicheza, kama beki wa kati.
Vile vile aliwahi kuifundisha Togo na Nigeria katika kombe la dunia, vile vile Mali.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video