Monday, June 20, 2016

CLEVELAND Cavaliers wamepambana mno kupata ubingwa wa NBA, Marekani kwa mwaka 2016. Na kwa hakika wamefanikiwa.
Mwiko umevunjwa. Kwa miaka 52 (yaani tangu mwaka 1964), Cavaliers walitamani kushinda taji la NBA bila mafanikio. Hawakuwa kwenye zama zao za ukubwa. Zilikuwa nyakati za mafahari wengine kupokezana mataji.
Mwaka jana (2015), Cavaliers (Cavs), walikaribia kufikia mafanikio waliyoyahitaji. Hata hivyo, katika mechi sita za fainali NBA, waliburuzwa na Golden State Warriors ambao walitawazwa machampioni.
Imetokea bila shaka kwamba Cavaliers na Warriors ndiyo wapinzani wenye nguvu kwa misimu miwili mfululizo. Mwaka huu wamekutana katika michuano mikali iliyowalazimisha kwenda michezo saba ya fainali.
Kama ilivyokuwa mwaka jana, Cleveland Cavaliers waliibuka kidedea kwa kutwaa ubingwa wa Mashariki (Eastern Conference) ligi ya NBA.
Ni utaratibu wa ligi ya NBA kugawa pande za mashindano. Mashariki na Magharibi kisha bingwa wa kila upande, hupambana kumpata bingwa wa jumla wa mashindano katika mwaka husika.
Hata hivyo, mwaka jana baada ya Cavs kufanya vizuri Eastern Conference, waliambulia patupu katika mbio za ubingwa wa kitaifa kwa kucharazwa vikapu vya kutosha katika michezo sita waliyokutana na mabingwa wa Magharibi (Western Conference), Golden State Warriors.
Cavaliers walishinda michezo miwili tu, wakipata pointi 95-93 (Juni 7, 2015) na 96-91 (Juni 9, 2015), wakati Warriors waliigeuza urojo Cavaliers na LeBron wao kwa pointi 108-100 (Juni 4, 2015), 103-82 (Juni 11, 2015), 104-91 (Juni 14, 2015) na 105-97 (Juni 16).
2016, umekuwa mwaka mzuri kwa Cavs, baada ya kushinda taji, ikiwa ni baada ya kupambana kwa jasho na moyo kutoka nyuma, kusawazisha kabla ya kuchukua uchampioni wa NBA ambao ni mtamu mno kwao.
SABABU ZA UBINGWA
Kila kitu hutokea kwa sababu. Mafanikio yoyote mtu huyapata kutokana na zile sababu ambazo alizitengeneza kuyaita.
Cavs waliyaita mafanikio yao mwaka 2016, hivyo ni sababu kubwa kufanikiwa lakini Warriors hawakupambana inavyotakiwa, hasa katika mechi tatu za mwisho.
Warriors walifikia kipindi ambacho walihitaji kushinda mchezo mmoja tu waweze kutangazwa mabingwa, walipokuwa wameshacheza michezo minne ya fainali lakini hawakupambana inavyotakiwa.
Nini kimeipa ubingwa Cavaliers mwaka huu? Yapo majibu matano ambayo yanathibitisha sababu za Cavs kutwaa uchampioni wa NBA mwaka huu, japo ilikuwa ni kwa kupambana kupita kiasi.
UBORA WA LEBRON JAMES
Humpendeza zaidi akiitwa King James. Amekuwa kwenye kiwango bora kwa wakati huu. Michezo mitatu ya mwisho, alionesha dhamira ya kweli ya kushindana hadi kushinda taji na kurejesha hadhi yake.
Haijashangaza kwa LeBron kutangazwa mchezaji bora wa fainali (MVP) na amekabidhiwa kikombe chake bila ubishi wowote.
LeBron alipohama kutoka Miami Heat msimu uliopita na kutua Cavs, wapo ambao walimbeza kuwa anajikweza sana, kwamba asingeweza kuisaidia chochote Cavaliers.
Hata hivyo, alfajiri ya leo, akiwa katika hisia kali ambazo zilisindikizwa na machozi, LeBron alisema: “Nilikuja Cavaliers ili kuling’arisha jiji letu (Cleveland), kuliondolea ukame wa kushinda taji la NBA.
“Malengo yangu yametimia. Tumefanikiwa, ilikuwa lazima tupambane na kweli tumepambana mpaka mwisho.”
LeBron alikuwa kwenye wakati mzuri wa kufunga vikapu, kurudi kuzuia, ‘kublok’ mipira iliyokuwa inakwenda kuwa vikapu kwenye goli lao, vilevile kucheza rebound. Kuhusu ku-dunk, LeBron ‘ali-dunk’ sana tu.
Kwa hakika, timu inapokuwa na mchezaji kama LeBron, tayari inakuwa imeshajihakikishia matokeo, kwani huhitajika nyongeza ndogo tu. Ubora wa LeBron ni sababu muhimu kwa Cavs kutawazwa machampioni wa NBA baada ya kupanga foleni kwa miaka 52.
UKUBWA WA MIILI YA CAVS
Cavaliers inaundwa na wachezaji wenye miili mikubwa. Walipokutana na Warriors, ilikuwa kama mijibaba inacheza na vivulana.
Kitu ambacho kimekuwa kikiwabeba Warriors ni ufundi ambao mchezaji mmoja-mmoja anao, ukijumlisha na uhodari wa mtaalamu mwenye shabaha za kutupia pointi tatu, Stephen Curry.
Katika michezo mitatu ya mwisho ya fainali, Cavs waliamua kutumia ukubwa wa miili yao, kuwabughudhi Warriors wasicheze mchezo wao, huku wao wakitumia faida yao ya miili nyumba kuwanyamazisha mafundi wenye nidhamu kutoka Western Conference.
Wakiwa na faida hiyo ya ukubwa wa miili, Cavs walihakikisha wanaziba mawasiliano ya Warriors uwanjani, hivyo kusababisha mafundi hao wa Western Conference wawe wanapoteza mipira mara kwa mara.
Kwa pointi hiyohiyo ya ukubwa wa miili, LeBron alijikabidhi jukumu la kumkaba Curry, akahakikisha hafurukuti, japo ilikuwa kazi ngumu kutokana na ufundi wa janki huyo asiye na makuu, lakini mwisho iliwezekana.
HAMASA YA LEBRON
Narudia tena, ukiwa na mchezaji kama LeBron, unakuwa unahitaji nyongeza ndogo ili ufanye vizuri, maana peke yake anaziba nyufa nyingi kwenye timu.
LeBron ni mfungaji, mzuiaji, mchezesha timu, mvuruga mipango ya wapinzani, mtoa pasi muhimu.
Peke yake huota mafanikio kisha kuwaambukiza wachezaji wenzake. Huwahamasisha wachezaji wenzake kwenye vyumba vya kubalishia nguo, nyakati za mapumziko na hata uwanjani.
Kile ambacho hukihamasisha kwa wenzake hukionesha kwa vitendo uwanjani. Ukiwa mchezaji wa kikapu na ukacheza timu moja na LeBron ni sawa na kuingia mchezoni na kocha ndani ya uwanja.
Mchezo wa nne ulipomalizika, Warriors walikuwa wanaongoza kwa games 3-1, LeBron alisema: “Ni lazima tupambane.” Kweli walipambana, na matokeo yameonekana.
NIDHAMU YA MCHEZO
Baada ya kumalizika kwa mchezo wa nne (game 4), Warriors wakiwa wanaongoza games 3-1, walijiona kama vile wameshachukua uchampioni wa NBA 2016, kwa kujumlisha historia ya mwaka jana.
Ikiwa imebaki michezo miwili, Warriors waliona hakukuwa na ugumu wowote kushinda mchezo mmoja kati ya hiyo. Kutokana na hali hiyo, waliingia uwanjani kama mabingwa tayari, wasiohangaika kutafuta matokeo.
Nidhamu hiyo ya kuingia mchezoni kama mabingwa, ilisababisha wapotee mchezoni dhidi ya Cavs ambao walipambana kufa au kupona kwa sababu walijua kuwa kupoteza mchezo maana yake ni kukubali kupoteza kombe kwa fainali ya pili mfululizo.
Hii ndiyo sababu kwenye mechi tatu za mwisho, Cavs walikuwe wenye kasi zaidi, huku wakitawala idara zote, wakati Warriors walibaki kufurukuta tu.
WARRIORS WALIKOSA PLAN B
Game 5 na 6, zilionesha kuwa jeuri ya Cavs ni miili mikubwa ambayo waliitumia kuwabughudhi na kuwazuia Warriors wasicheze mchezo wao. Vilevile kuziba nafasi kati ya mchezaji wa Warriors na mwingine, hivyo kuwapotezea mawasiliano.
Pasi za juu ziliwashambulia Warriors, maana mara zote walipoteza mipira kwa sababu Cavs ni warefu zaidi, wakati pasi za viuno hazikuwa na matokeo kwa kuwa Cavs waliziba njia. Ukubwa wao uliwafanya waonekane wengi uwanjani kuliko Warriors.
Warriors waliingia game 7 wakiwa na mbinu zilezile, hivyo kuwapa urahisi Cavs kuwabana kama kawaida kisha kuwashambulia kwa kasi zaidi na kupata ushindi. Kimsingi katika game 7, Warriors walionekana kukosa plan B, baada ya kuzidiwa kimchezo katika game 5 na 6.
Credit: Ndimi Luqman Maloto

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video