Wednesday, June 15, 2016

Cristiano Ronaldo ni mchezaji mkubwa sana ulimwenguni, lakini wakati mwingine huwa anaharibu heshima yake kutokana na matendo na kauli zake. Yeye huwa anaamini katika kupata matokeO chanya na si vinginevyo. Hilo si tatizo.
Wachambuzi wa masuala ya soka wamesema kitendo cha mchezaji wa aina yake kuzungumza maneno yasiyo ya kimichezo dhidi ya Iceland katika mchezo wa jana, ambapo timu yake ya Ureno ilibanwa mbavu na kutoka sare ya bao 1-1 katika michuano ya Euro mchezo wa kundi F hakikuwa cha kiungwana.
Kutokana na uchanga wa taifa la Iceland katika nyanja ya michezo barani Ulaya, Ronaldo alipaswa kuwapongeza badala ya kuwatolea maneno ya kejeli....baada ya mchezo wa jana, Ronaldo alikaririwa akisema.
“Iceland walikuwa na lengo la kujilinda tu...walipata nafasi mbili lakini hata hawakujaribu kufunga. Baada ya sare waliyopata walisherehekea mithili wamechukua ubingwa wa Euro au kitu gani sijui, hiyo ni akili ndogo. Na ndiyo maana hawatafanya chochote katika michunao hii."

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video