Shabiki wa kugalagala wa Yanga, Ridhiwani Kikwete amesema amejitokeza kusema wazi iwapo Yusuf Manji atachukua fomu kugombea tena nafasi ya mwenyekiti, yeye atakuwa kati ya watakaompa kura.
Ridhiwani ambaye ni Mbunge wa Chalinze (CCM), amesema ameridhishwa na mafanikio iliyoyapata Yanga ikiwa chini ya Manji.
“Niwe mkweli kabisa Yanga imekuwa na maendeleo mazuri chini ya uongozi wa bwana Manji. Hili linanifanya kura yangu iwe kwake kama ataamua kuendelea kugombea,” alisema Ridhwani.
Manji anatarajia kuchukua fomu leo katika uchaguzi ambao utafanyika Juni 11 jijini Dar es Salaam.
Chanzo:Salehjembe.
0 comments:
Post a Comment