Mchezaji wa Mtibwa Suger, Shiza Kinyuya akipokea hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 1/-toka kwa Ofisa Udhamini na Matukio wa Vodacom Tanzania, Ibrahim Kaude(kushoto)baada ya kuibuka mchezaji bora wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara mwezi April 2016,Makabidhiano hayo yalifanyika jana katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Katikati ni Ofisa wa Ligi,Joel Balisiya.Ofisa Udhamini na Matukio wa Vodacom Tanzania, Ibrahim Kaude akimkabidhi hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 1 Mchezaji wa Yanga, Juma Abdul, baada ya kuibuka mchezaji bora wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara mwezi Mei 2016,Makabidhiano hayo yalifanyika jana katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katikati Ofisa wa Ligi, Joel Balisiya.Mchezaji wa Mtibwa Suger,Shiza Kinyuya akiwa ameshikilia hundi yake yenye thamani ya shilingi Milioni 1/=baada ya kukabidhiwa rasmi na wadhamini wakuu ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania jana katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ya kuwa mchezaji bora wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara mwezi April 2016.
Friday, June 3, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment