Monday, June 13, 2016

Mabingwa wa dunia timu ya taifa ya Ujerumani wameanza michuano ya Ulaya kwa rekodi kwa kuinyuka Ukraine.

Ukiachilia mbali kiwango cha juu kilichooneshwa na Toni Kroos na goli la mapema la kichwa lililofungwa na Shkodran Mustafi, bado safu yao ya ulinzi ilifanya makosa mara kadhaa.

Jerome Boateng aliokoa mpira kwenye mstari wakati golikipa wa Ujerumani Manuel Neuer akifanya kazi ya ziada kuokoa michomo ya hatari kabla ya kupata bao la pili kwenye dakika za hatari.

Yevhen Konoplyanka alikuwa mwiba kwenye ngome ya Ujerumani lakini hata hivyo juhudi zake za kuitafutia Ukraine bao la kusawazisha ziliota mbawa kufuatia Bastian Schweinsteiger kuingezea Ujerumani bao la pili katika dakika za lala salama.

Kiungo huyo wa Manchester United ambaye hajacheza tangu March 20 kutokana na majeraha ya goti, aliingia kipindi cha pili akitokea benchi katika dakika za mwisho na dakika mbili baadaye akafunga bao tamu lililotokana na shambulizi la counter attack.

Baada ya Poland kuichapa Ireland ya Kaskazini siku ya Jumapili, Ujerumani sasa wanakaa kileleni kwa Kundi C. Alhamisi Ujerumani itacheza mchezo wake wa pili dhidi ya Poland ambapo Ujerumani ilichezea kichapo walipokutana kwenye mechi za kuwania kufuzu kwa Euro 2016.

Licha ya ushindi, Ujerumani hawajaonesha kiwango kilichotarajiwa na wengi

Ikiwa imepoteza mechi saba kati ya 18 tangu ilipotwaa ndoo ya World Cup kwenye ardhi ya Brazil miaka miwili niliyopita pamoja na vichapo kutoka kwa Jamhuri ya Ireland na England mabingwa hao maratatu wa kombe la michuano ya Ulaya wameonekana sio wagumu kama ilivyokawaida.

Kulikuwa na wakati kikosi chao kilionekana kufunguliwa na mashambulizi ya Ukraine ambao walikuwa hawajawafunga kwenye mechi tano zilizopita.

Ujerumani huenda wangepata bao kutokana na free-kick iliyozua utata baada ya Yaroslav Rakitskiy kuonekana kaucheza mpira licha ya kumfanyia- tackling Thomas Muller.

Hata hivyo, Neuer alikuw busy muda mwingi kwenye milingoti mitatu ya Ujerumani huku Boateng akiiokoa timu yake kwa kuokoa mpira katikati ya mstari azima juhudi za Konoplyanka kuipatia Ukraine bao.

Mario Gotze alisahaulika ndani ya uwanja huku akiwa ndiye mchezaji pekee mwenye touches chache uwanjani. Viungo Muller na Mesut Ozil hawakuwa kwenye ubora wao uliozoeleka licha ya kiungo wa The Gunners kupiga krosi iliyounganishwa vyema kambani na Schweinsteiger.

Kikosi cha Joachim Low kilizidi kufunguliwa kwenye safu ya ulinzi kadiri muda ulivyokwenda mbele, na kuna haja ya kikosi hicho kufanya marekebisho makubwa wakati michuano hiyo ikiendelea kabla haijakutana vidume vingine vya Ulaya.

Kama kiungo mwenzake wa Real Madrid Luka Modric, ambaye alikuwa chachu ya ushindi wa Croatia dhidi ya Uturuki kwenye mchezo wa mapema, Kroos alicheza kwa kujiamini huku akiwa na kumbukumbu ya kushinda ndoo ya klabu bingwa Ulaya mwezi uliopita.

Si tu alikuwa boss wa mchezo tangu ulipoanza, lakini mpira wake wa adhabu ndongo ulitua moja kwa moja kichwani kwa Mustafi ambaye aliifungia Ujerumani bao la kuongoza dakika ya 19 baada ya kuanza kwa mchezo huo.

Pasi-kisu nyingine kutoka kwa kiungo huyo mchezeshaji wa zamani wa Bayern Munich ingeweza kupelekea Ujerumani kupata bao la pili lakini shuti la Sami Khedira lilikwenda moja kwa moja kwenye mikono ya golikipa wa Ukraine Andriy Pyatov.

Nyota huyo mwenye miaka 26 mpira wake uligongonga mtambaa panya dakika za mapema kipindi cha pili na hiyo ilidhihirisha kwamba kiwango chake kinaweza kuwa msaada mkubwa kwa timu yake kufanya vizuri kwenye michuano ya Euro 2016 nchini Ufaransa.

Ukraine walimpa nafasi kubwa ya kufanya kila alichojisikia kufanya, lakini huenda timu nyingine zisimpe nafasi hiyo kutokana na kumkaba vilivyo ili kukata mirija ya usambazaji wa mipira kwenye kikosi cha Ujerumani.

Dondoo muhimu
  • Shkodran Mustafi amefunga goli lake la kwanza tangu aanze kuichezea timu ya taifa ya Ujerumani ikiwa ni mchezo wake wa 11
  • Joachim Low ameiongoza Ujerumani kushinda mchezo wa 88 akiwa kama kocha, Sepp Herberger pekee ndiye anayemzidi ambaye alikiongoza kikosi cha Ujerumani kushinda michezo 94.
  • Ujerumani imecheza michezo 12 imeshinda 7 na kutoka sare mara 5, haijapoteza mchezo kwenye mechi zake za ufunguzi za michuano ya mataifa ya Ulaya. IImeshinda mechi nyingi za ufunguzi zaidi ya nchi yoyote.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video