Monday, June 13, 2016

Michuano ya Euro inaendelea tena leo ambapo mbali na michezo mingine, mchezo kati ya Uhispania ya Jamhuri ya Czech utakuwa na uhondo wa aina yake. Huu ni mchezo wa kundi D ambao utachezwa majira ya saa kumi alasiri kunako dimba la Stadium de Toulouse lililopo manispaa ya Tolouse.
Katika mchezo huu Uhispania anaingia kama bingwa mtetezi, lakini ambaye amekuwa hana rekodi ya kuridhisha sana.
Walitolewa katika hatua ya makundi kwenye michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2014 nchini Brazil, lakini licha ya hayo yote rekodi yao katika michuano hii bado si haba hasa ukizingatia wao ndio walichukua mwaka 2008 walipoifunga Ujerumani 1-0  na kisha kulitetea tena mwaka 2012 baada ya kutoa kipigo cha mbwa mwizi cha mabao 4-1 dhidi ya Italy.
Wachambuzi wa mambo ya soka wanaichambua Uhispania kama taifa ambalo siku za hivi karibuni limepoteza uwezo wa mchezaji mmoja mmoja, hali ambayo imekuwa ikiinyima matokeo mazuri sana ukilinganisha na nyakati za nyuma.
Mchezo wao wa mwisho wa kirafiki walifungwa bao 1-0 dhidi ya Georgia.
Jamhuri ya Czech vile vile si timu ya kubeza, kwani wana rekodi ya aina yake licha ya kutowahi kutwaa taji hili. Mwaka 1996 waliamaliza katika nafasi ya pili huku mwaka 2004 wakitolewa kwa mbinde na wenyeji Ugiriki katika hatua ya nusu fainali wakati huo wakiwa na kikosi chenye wachezaji wenye vipaji vya aina yake kama Jan Koller, Pavel Nedvěd, Milan Baroš na wengine wengi.
Baada ya hapo walianza kupotea taratibu lakini kazi nzuri chini ya kocha Pavel Vrba imeanza kurudisha makali ya Czech, ambapo wamekuwa wakitoa ushindani wa hali ya juu kwenye kila mchezo.

Taarifa muhimu kutoka kila timu.
Kipa wa Uhispania David De Gea anakabiliwa na shutuma za ya ngono ambazo zimesambaa kwenye vyombo vingine vya habari nchini kwao, licha ya yeye mwenyewe kukanusha vikali.
Lakini inaonekana bado kocha ana imani naye na hivyo kumpa nafasi ya kukaa langoni leo mbele ya mkongwe Iker Casillas.
Alvaro Morata ataongoza safu ya ushambuliaji baada ya kupona maumivu yake ya nyama za paja.
Kwa upande wa Jamhuri ya Czech, ambao walifuzu juu ya timu za Iceland, Uturuki, Uholanzi na Vrba wako kamili kabisa wakiongozwa na nahodha wao Tomas Rosicky.

Makocha wanasemaje?
Kocha wa Uhispania Vicente del Bosque anasema: "Hatupaswi kuweka ukomo wa kufika hatua fulani katika michuano hii. Hatuwezi kusema kwamba labda tukifika nusu fainali tutafurahi, tunahitaji kupambana ili kushinda kila mchezo. Huu ni mchezo, hivyo hatuwezi kujua tutafika hatua gani, lakini muhimu ni kuhakikisha tunapigania ndoto zetu za kutwaa kombe hili kwa mara ya tatu mfululizo".

Kocha wa Jamhuri ya Czech Pavel Vrba anasema: "Timu yao (Uhispania) imeundwa na wachezaji bora ulimwenguni ambao wanatoka Barcelona na Real Madrid. Hivyo utakuwa ni mtihani mgumu sana kwetu , lakini tutajitahidi kadri ya uwezo wetu kupambana nao na naamini tutaweza licha ya kwamba kutakuwa na ugumu mkubwa".

Dondoo muhimu
  • Uhispania hawajafungwa na Czech kwenye michezo minne waliyokutana tangu uhuru wao (wameshinda mara tatu, sare moja). Wameshinda mechi zote tatu za mwisho walizokutana.
  • Katika michezo 12 ambayo Uhispani walikutana na iliyokuwa Czechoslovakia iliisha hivi (ushindi mara 4, sare 1, kufungwa 7...ushindi mara 2 na kufungwa mara 3 katika michezo ya kimashindano).
  • Uhispania walifuzu Kombe la Dunia mwaka 1998 kwa makosa ya Jamhuri ya Czech. 
  • Pindi timu hizi zilipokutana wakati wa kufuzu UEFA EURO 2012. Uhispania ilishinda 2-1, magoli yakifungwa na David Villa katika mchezo wa awali uliochezwa Granada. Mchezo wa pili uliochezwa nyumbani kwa Czech, waliibuka tena na ushindi wa magoli 2-0 yakifungwa na Juan Mata na Xabi Alonso 
  • Hii ni mara ya sita mfululizo Uhispania wanashiriki michuano hii, wanapigana kuchukua kombe kwa mara ya tatu mfululizo baada ya kuwa timu ya kwanza kuchukua mara mbili mfululizo mwaka 2008 na 2012.
  • Uhispania na Ujerumani ndio timu zenye mafanikio makubwa kwenye michuano hii. Wamchukua ubingwa huu mara 3
  • Tangu Jamhuri ya Czech kupata uhuru wao hawajawahi kukosa kushiriki kwenye michuano hii.
  • Waliwahi kushinda taji la michuano hii mwaka 1976, wakati huo wakiwa sehemu ya Czechoslovakia na kufanikiwa kufika fainali kwa mara ya kwanza kama taifa la Jamhuri ya Czech mwaka 1996 ambapo walifungwa na Ujerumani.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video