Monday, June 27, 2016

Leo ni kama mtoto hatumwi dukani katika michuano ya Euro inayoendelea nchini Ufaransa wakati miamba miwili ya Italy na Uhispania itakapokuwa ikiumiza nyasi za uwanja wa Stade de France jijini Paris, mchezo utakaofanyika majira ya saa 1 za usiku.
Timu hizi zimeingia katika hatua hii ya 16 bora zikiwa na pointi sawa lakini nafasi tofauti. Italy walimaliza vinara katika kundi lao baada ya kujikusanyia alama sita mbele ya timu za Ubelgiji, Ireland na Sweden wakati Uhispania wameingia baada ya kumaliza nafasi pili nyuma ya Croatia na mbele ya Uturuki na Jamhuri ya Czech.
Katika mchezo wa leo Italy wanaweza kuanzisha wachezaji 10 kati ya 11 walioanza kwenye mchezo wao wa ufunguzi dhidi ya Ubelgiji.
Antonio Candreva atakuwa nje kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya paja na nafasi yake inaweza kujazwa na nyota wa AS Roma Alessandro Florenzi.
Uhispania wanataraji kuanzishwa kikosi kizima ambacho kimekuwa kikianza kwenye mchuano hii.
Nahodha Sergio Ramos ana kadi ya njano na endapo atapata tena kadi nyingine basi yuko hatarini kukuso mchezo wa robo fainali endapo timu yake itafuzu.
Pambano hili ni zito mno kwani linaikutanisha miamba miwili ambayo pia ni mahasimu wakubwa katika eneo la Mediterranea.
Hii inakuwa ni mara ya sita kwa Italy kukutana na Uhispania katika fainali hizi za michuano ya Ulaya, na kuvunja rekodi ya timu mbili kukutana mara nyingi zaidi katika michuano hii. Hii inakuwa ni mara ya nne tangu mwaka 2008.
Kuelekea pambano hili, Uhispania wanawachukulia mahasimu wao 'Azzurri' kama  watu wa kuogopwa sana, sio kwa sababu ya ubora wao kimbinu bali kwasababu ya uwezo wao mkubwa wa kuusoma mchezo, safu bora ya ulinzi na uwezo wa kuwalazimisha wapinzani kucheza kama wanavyotaka.
Uhispania walivunja mwiko wa muda mrefu wa kutoifunga Italy kwenye michuano mbalimbali mwaka 2008 pale walipowachapa kwa matuta na baadaye kuwapa kipigo cha mbwa mwizi kwenye fainali ya mwaka 2012 kufuatia kuwatandika mabao 4-0.
Beki wa Italy Giorgio Chiellini anatambua ubora wa wapinzani wao kwa sasa na kukiri kwamba kwa sasa Uhispania ni timu hatari mno kwao.
"Ubora wao ulianza wakati walipotufunga kwenye michunao ya Euro mwaka 2008," Chiellini amesema.
"Mchezo ambao tulishindwa kabisa kuwapa upinzani ulikuwa ule waliotufunga mabao 4-0 jijini Kiev kwenye fainali ya Euro mwaka 2012 kutokana na kushindwa kurudi katika ubora wetu baada ya kazi nzito kwenye mchezo dhidi ya Ujerumani."
"Lakini yote kwa yote mchezo wa Jumatatu (leo) utaamuliwa na matukio kwa pande zote mbili."

Takwimu za michezo waliyokutana.
  • Katika michuano mitatu iliyopita ya Euro, timu hizi zimekutana mara nne huku jumla zikikutana mara sita, wakiweka rekodi ya kuwa timu zilizokutana mara nyingi zaidi kwenye michuan hii. 
  • Ushindi wa mara ya mwisho kwa Italy dhidi ya Uhispania katika michezo ya ushindani ulikuwa ni wa mabao 2-1. Ilikuwa katika mchezo wa robo fainali ya Kombe la Dunia mwaka 1994. Kocha wa Italy Antonio Conte wakati huo akiwa mchezaji alianza mchezo huo.
  • Tangu hapo, Uhispania wamepoteza mechi 11 dhidi ya Italy (zikiwemo za Kirafiki), wakishinda mara nne na kutoka sare mara sita (michezo miwili walioshinda kwa penati imehesabiwa kama sare).
Italy
  • Kipigo kutoka kwa Jamhuri ya Ireland kilikuwa ni cha kwanza kwa Italy kwenye michezo 13 ya ushindani chini ya Antonio Conte (wameshinda mara 9, sare mara 3)
  • Italy wameshindwa kufunga kwenye michezo mitatu kati ya minne ya mtoano ya Michuano ya Ulaya, ukiachana na ule walioshinda 2-1 dhidi ya Ujerumani katika hatua ya nusu fainali mwaka 2012.
  • Italy wametumia wachezaji wengi zaid katika hatua ya makundi (22), ukujumuisha wachezaji wote 20 wa ndani Ni Leonardo Bonucci na Andrea Barzagli pekee ndio wameanza katika michezo yote mitatu
  • Italy hawajawahi kufunga zaidi ya magoli mawili katika michezo yao 36 iliyopita kwenye Michuano ya Ulaya.
  • Kipigo cha leo kitapelekea Italy kupoteza mechi mbili mfululizo kwenye Michuano ya Ulaya kwa mara ya kwanza.
Uhispania
  • Uhispania wamepoteza wamepoteza michezo mitatu kati ya sita ya mwisho katika Michuano ya Kombe la Dunia na Ulaya, mara nyingi zaidi kwenye michezo yao 31 iliyopita katika michuano mbalimbali.
  • Kati ya mashuti 48 aliyopiga Sergio Ramos katika Michuano ya Kombe la Dunia na Ulaya, hakuna hata moja lililolenga lango (ukiondoa mikwaju ya penati).

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video