Sunday, June 5, 2016

Ni huzuni ya aina yake, huzuni kwa ulimwengu wa wapenda michezo wote hasa ndondi baada ya kumpoteza moja ya wanamasumbwi hodari kuwahi kutokea duniani Muhammad Ali.
Muhammadi Ali alikuwa ni kipenzi cha watu wote waliokuwa wanatambua thamani ya michezo ulimwenguni. Amefikwa na umauti jana katika hospitali ya Phoenix, iliyopo Arizona alipokuwa amelazwa tangu Alhamisi kutokana maradhi ya mapafu yaliyokuwa yakimsumbua. Amekufa akiwa na umri wa miaka 74.
Kwa muda mrefu, Ali alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya mwili kutetemeka (Parkinson disease) ambayo yalimuanza mwaka 1981.
Kwa mujibu wa familia yake, Ali atazikwa nyumbani kwake huko Louisville, Kentucky.
Salamu za rambirambi kutoka viongozi mablimbali pamoja na watu maarufu ulimwenguni zimekuwa zikimiminika kutokana na historia kubwa aliyoacha Ali katika ulimwengu huu.
Barack Obama, rais wa Marekani na mkewe Michelle Obama wamesema "Muhammad Ali aliuteka na kuushtua ulimwengu. Na ulimwengu unajivunia kwa hilot".
Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton amesema: Ali alikuwa ni mwenye hamasa aiwa ulingoni, na kuwavutia vijana, na wote waliokuwa wakiupenda mchezo huo".
Mgombea urais wa Marekani kupitia Republican  Donald Trump, kwenye twitter yake aliandika hivi:  Ali alikuwa ni bingwa wa ukweli na kijana wa aina yake. Atakumbukwe na watu wotel!".
Don King ambaye amewahi kusimamia mapambano mengi ya Ali liliwemo la 'Rumble in the Jungle' amesema: "Ni siku ya huzuni kubwa katika maisha, Nilimpenda Muhammad Ali, alikuwa ni rafiki yangu. Kamwe Ali hatakufa, kama ambavyo ilivyo kwa Martin Luther King, nafasi yake itabaki kwa sababu alisimama kwa maslahi ya ulimwengu".
George Foreman ambaye alikuwa mpinzani wake katika pambano la 'Rumble in the Jungle' amesema: "Muhammad Ali alikuwa moja ya wanadamu wa tofauti sana ambao nimewahi kukutana nao. Hakuna shaka kwamba alikuwa mmoja wa watu bora kabisa kuwahi kuishi naye katika umri na siku hii". 
George Foreman, ambaye ambaye alipoteza ubingwa wake dunia kwa Ali katika pambano lilipachikwa jina la "Rumble in the Jungle" lililofanyika Kinshasa mwaka 1974, aliwahi kusema kwamba, Ali ni moja katika ya binadamu wa kipekee ambao amewahi kukutana nao.
Mwanaharakati wa haki za binadamu nchini Marekani Jesse Jackson alisema Ali alithubutu kuutoa sadaka ubingwa wake na pesa kutokana na kusimamia misingi yake dhidi ya vita ya Vietnam.
Ali ambaye alizaliwa mwaka Januari 17, 1942 wakati huo akijulikana kwa jina la Cassius Marcellus Clay, alianza kuonesha mwanga wa mafanikio katika 'career' yake mwaka 1960 pale ambapo alishinda ubingwa wa uzito wa juu-mwepesi katika michuano ya Olimpiki iliyofanyika Rome nchini Italy.
Akiwa amepachikwa jina la "The Greatest", Ali alimpiga  Sonny Liston mwaka 1964 na kushinda kwa mara ya kwanza ubingwa wa dunia wa uzito wa juu na kuwa bondia wa kwanza kutwaa ubingwa wa dunia wa uzito wa juu katika maeneo matatu tofauti.
Ali alistaafu ndondi mwaka 1981, akiwa ameshinda mapambano 56 katika ya 61 aliyocheza.
Ali alitunukiwa tuzo ya mwanamichezo bora wa karne na BBC. Alijulikana sana kwa maneno yake makali kabla na baada ya mchezo na kutabiri matokeo kutokana na namna alivyojaaliwa uwezo wa kupigana akiwa ulingoni.
Atakumbukwa kwa kuwa kiongozi katika kupigania haki za binadamu, hasa haki za watu weusi ambao wakati huo walikuwa wakinyanyasika nchini Marekani.
Moja ya majibu ya kipekee kuyatoa ni pale alipoulizwa kwa namna gani angependa akumbukwe pindi atakapokuwa hayupo duniani....alisema: Nataka nikumbukwe kama mtu ambaye hakuwatupa watu wake. Lakini kama hilo ni kubwa sana, basi nikumbukwe kama bondia bora.
"Hata hivyo sitajali kama hutotaja namna gani nilikuwa mwema."
Ali aligeuka kuwa bondia rasmi wa ngumi za uzito wa juu katika michunao ya Olimpiki iliyofanyika Rome kutokana na uwezo wake mkubwa wa kurusha makonde mazito.
Bondia Bingwa wa Uingereza wakati huo Henry Cooper alijitahidi kupambana na Ali na kukaribia kumshinda wakati huo Ali alikuwa hajulikani sana pindi walipopambana mwaka jijini London mwaka 1963. Hata hivyo Cooper alisukumiwa konde zito na Ali katika jicho la kushoto na kupelekea bondia huyo kustaafu.
Mwaka mmoja baadaye (1964), Ali alifanikiwa kushinda kwa mara ya kwanza ubingwa wa uzito wa juu duniani akiwa na miaka 22 baada ya kumtwanga Mmarekani mwenzie Sonny Liston.
Katika pambano hilo, alitabiri kumpiga Liston, ambaye kwa wakati huo alikuwa hajapoteza hata pambano moja, lakini Ali aliamini angemuadabisha na hakika alifanya hivyo.
Ilikuwa ni katika raundi ya sita Liston alisalimu amri na kukubali kichapo kutoka kwa Ali ambaye wakati huo alikuwa ni kijana mdogo sana.
Wakati wa pambano lake la kwanza dhidi ya Liston, Ali alikuwa ameshaanza kujihusisha na Nation of Islam, ambayo ilikuwa ni taasisi ya kidini ilikuwa na malengo ya kuwakomboa kiimani, kijamii na kiucnhumi Waafrika wote waliokuwa wakiishi Marekani.
Baadaye aliamua kubadilisha dini na kuwa Muislamu, na kuachana na jina lake la awali la Cassius Marcellus Clay ambalo aliita kama "slave name" na kutumia jina la Cassius X kabla ya kubdabilisha tena na kuitwa rasmi Muhammad Ali, jina ambalo amelitumia mpaka umauti wake.
Mwaka 1967, Ali aliamua kuchukua maamuzi magumu ya kukataa kujiunga na jeshi la Marekani lilikuwa likienda kupambana na Vietnam, suala ambalo lilipingwa vikali na Wamarekani wenzake. Alikataa kufanya hivyo kwa sababu muhimu sana, kwamba hawezi kwenda kuwaua raia wa Vietnam wakati hawajawahi kumuita 'Nigga' wala 'slave', na akasisitiza kuwa wazungu wa kimarekani walioanzisha vita dhidi ya Vietnam ndio wamekuwa wakiwatesa watu weusi nchini Marekani, akakataa kuwaunga mkono kwenye vita hiyo.
Tukio hilo lilisababisha kupokonywa ubingwa wake wa dunia na leseni yake ya ngumi, hali iliyopelekea kutopambana kwa miaka minne kutokana hapo awali kuhukumia kifungo cha miaka mitano jela. Hata hivyo,  mwaka  1974 alikata rufaa na kushinda baada ya kutumikia miaka minne gerezani, aliporudi uraiani hakuruhusiwa kusafiri nje ya nchi lakini baadaye leseni yake ilirejeshwa.
Pambano la kwanza kwa Ali kupoteza lilikuwa dhidi ya Joe Frazier, pambano ambalo lilipachikwa jina la "Fight of the Century" lillilofanyika New York March 8 mwaka 1971.
Lakini baadaye alirejesha heshima yake baada ya kumtwanga George Foreman kwa 'knock out' (KO) raundi ya nane katika pambano lililopachikwa jina la "Rumble in the Jungle" lililopigwa Kinshasa, Zaire (kwa sasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC)) Oktoba 30, mwaka 1974.
Katika pambano la kukumbukwa zaidi katika historia ya maisha ya Ali ni lile dhidi Frazier ambalo walikuwa wakipigana kwa mara ya tatu na ya mwisho Ufilipino Oktoba 1 1975. Katika Pambano hilo ambalo lilijulikana kama "Thrilla in Manila" Frazier alishindwa katika raundi ya 15 baada ya wasaidizi wake kurusha taulo. 
Baada ya pambano hilo, Ali alisema kwamba ushindi wake umetokana na wasaidizi wa Frazier kuwahi kuomba mwamuzi amalze pambano, kwani yeye pia alidai huenda asingeweza kuendelea kumalizia raundi ya mwisho kutokana na uchovu aliokuwa nao.
Baada ya hapo, mwaka 1978 Ali alipigwa na Leon Spinks na baadaye kupigwa tena na  Larry Holmes mwaka 1980 pamoja na Trevor Berbick mwaka 1981. Wachambuzi wa masuala ya ndondi walisema kuwa Ali alipaswa kustaafu kabla ya hapo kutokana na mwili wake kuanza kuchoka. Baada ya hapo ndipo alipoanza kusumbuliwa na maradhi ya maradhi ya Parkinson.
Alipigana jumla ya mapambano 61. Alipigwa mara tano tu. Alishinda mapambano 37 kwa knockout.

Namna gani Ali alipenda watu wamkumbuke.
"Ningependa kukumbukwa kama mtu ambaye nimeshinda ubingwa wa dunia wa uzito wa juu mara tatu, ambaye nilikuwa mcheshi na niliyemtendea haki kila mtu.
"Kama mtu ambaye nilipenda kujishusha kwa wote walionipandisha...ambaye alisimama thabiti kupigania imani yake...ambaye alijitahidi kuwaunganisha watu wa aina zote kwa imani na upendo.
"Kama hayo yote ni makubwa sana, basi nadhani ningependa kukumbukwa tu kama bondia mkubwa ambaye nilikuja kuwa kiongozi na bingwa wa watu wangu. na sitajali pia kama watasahu mema yote aliyofanya".

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video