Sunday, June 5, 2016

Mayanga (kushoto) na Mecky Mexime.
Uongozi wa Mtibwa Sugar umesita kulizungumzia suala la kutaka kumrejesha kikosini Salum Mayanga ambaye sasa anakinoa kikosi cha Prisons ya Mbeya.
Kumekuwa na taarifa kwamba Mtibwa Sugar imeamua kumrudisha Mayanga aliyewahi kuwa bosi wa kocha wa sasa wa Mtibwa, Mecky Maxime ambaye imeelezwa anapelekwa Kagera Sugar.
Mratibu wa Azam FC, Jamal Bayser amesema kuwa kwa sasa wasingependa kulizungumzia suala hilo.
“Wewe umesikia wapi,” alihoji Bayser wakati akiongea na Salehjembe.
Alipoelezwa, kamwe huwa watoa habari hawatajwi, akasema:
“Nisingependa kulizungumzia suala hilo, kwanza sasa ni mapema sana.”
Imeelezwa kwamba Mtibwa Sugar wanataka kujiimarisha zaidi ili kuingia kwenye kundi la timu zinazowania ubingwa.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video