Monday, June 13, 2016

Mshambuliaji aliyekuwa anasakata kandanda katika klabu ya Mwadui FC, Jamal Simba Mnyate..hatimaye amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Simba sc Msimu ujao wa ligi kuu soka Tanzania bara.
Mnyate ameiambia MPENJA SPORTS mchana huu kwamba alichelewa kusaini kwasababu kuna mambo walishindwa kufikia muafaka.
"Siku chache zilizopita nilikuja Dar kusaini, lakini tulishindwa kukubaliana na nikarudi Nyumbani Morogoro, Jana nilikuja Dar, nimesaini mkataba wa miaka miwili baada ya kuelewana. Kwahiyo kila kitu tayari na nimerudi zangu Morogoro, ila kila kitu fresh kabisa na Simba". Mnyate ameithibitishia MPENJA SPORTS.
Hata hivyo, Mnyate hajaweka wazi dau alilopewa na Wekundu wa Msimbazi, lakini taarifa za awali zilieleza kwamba Simba walimtengea milioni 15.
Usajili wa Mnyate unaaminika kuwavutia mashabiki wengi wa Simba na wakati tetesi zikitawala kwamba atatua Msimbazi, wengi wao walisifia.
Pia huenda ilichangiwa zaidi na bao lake ambalo aliwafungia Mwadui kwenye ushindi wa 1-0 dhidi ya Simba katika mechi ya raundi ya pili ya ligi kuu Tanzania bara, uwanja wa Taifa.
Simba pia imemsajili mlinzi wa Mwadui, Emmanuel Simwanza, ingawa kamati ya Usajili ya klabu hiyo inasema mambo yao ni kimya kimya.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video