Kumradhi kwa taarifa ya awali kwamba Mnyate alikuwa amesaini Simba, ni kutokana na sintofahamu zilizotokea kutoka kwenye vyanzo vyetu vya habari...lakini taarifa kamili nii hapa......
MSHAMBULIAJI wa Mwadui FC, Jamal Mnyate amesema muda wowote kuanzia sasa atasaini mkataba wa miaka miwili Simba.
Mnyate amemaliza mkataba na Mwadui FC ambapo nao wako katika harakati za kumuongezea mkataba kwa msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Mnyate alisema bado hajasaini mkataba na Simba lakini wako katika mazungumzo na uongozi wa klabu hiyo na kila kitu kipo sawa.
"Bado sijasaini mkataba na Simba, ila nipo katika mazungumzo na muda wowote kuanzia sasa nitasaini mkataba na Simba," alisema
Mnyate alisema viongozi wa timu hiyo wamemtua nauli kutoka morogoro kuja jijini kwa ajili ya kusaini mkataba.
Alisema anatarajia kuja jijini kesho (jumapili) ambapo akifika ataenda kukutana na viongozi wa klabu hiyo.
0 comments:
Post a Comment