Friday, June 3, 2016

Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania Charles Boniface Mkwasa leo June 3 amekutana na waandishi wa habari kuelezea hali ya kikosi chake pamoja na mipango kuhakikisha Stars inaiuka na ushindi kwenye mchezo wake wa kesho dhidi ya Misri katika harakati za kuwania kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika mwaka 2017.

Mkwasa amesema, kila mmoja anatambua Misri ni timu ngu na wao wanaliheshimu hilo. Amesema mchezo wa kesho ni kama fainali kwa timu yake kwasababu inahitaji ushindi kwa kila njia.

“Tutapanga kikosi imara zaidi chenye lengo la kushambulia zaidi kwasababu tunahitaji tupate matokeo, hii mechi ni muhimu kama fainali na tunatambua tunacheza na timu ngumu. Tunawaheshimu Misri walitufunga magoli matatu kwao lakini kwenye mpira lolote linaweka likatokea”.

“Tunatambua kwamba tunadeni kubwa kwa watanzania na sisi kama wawakilishi wao tunahitaji kupata matokeo mazuri kwa ajili ya faraja kwa watanzania na pia kufungua njia kujaribu kuona tunaweza kupata nafasi ya kwenda hatua nyingine. Tunajua mechi itakuwa ngumu lakini tumejipanga kupambana nayo, tuko nyumbani, yale makosa ambayo tumekuwa tukiyafanya kwenye mechi za nyuma tumeyafanyia kazi”.

Stars ipo kundi G lenye timu tatu sambamba na Misri na Nigeria baada ya Chad kujitoa. Misri inaongoza kundi hilo ikiwa na pointi 7 baada ya kucheza michezo mitatu ikifuatiwa na Nigeria yenye pointi 3 ikiwa imecheza mechi tatu wakati Stars yenyewe ipo nafasi ya mwisho ikiwa na pointi moja baada ya kucheza mechi mbili. Matokeo hayo ni baada ya Chad kujitoa.

Hadi sasa bado haina goli hata moja katika mechi mbili, mechi ya kwanza ilifungwa magoli matatu na Misri ikiwa ugenini kabla ya kupata sare ya bila kufungana dhidi ya Nigeria.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video