Monday, June 27, 2016

Lionel Messi bado anasubiri taji lake la kwanza akiwa na timu ya taifa ya Argetina.

Messi aliushuhudia mkwaju wake wa penati unapaa juu ya ‘mtambaa panya’ kisha Francisco Silva akakwamisha mkwaju wa mwisho wa Chile na kushinda ubingwa wa Copa America kwa mara ya pili mfululizo kwa kuifunga Argentina kwa jumla ya penati 4-2 baada ya sare ya bila kufungana kwenye mchezo uliokwenda hadi dakika 120.

Akicheza mchezo wa fainali siku mbili baada ya kushrekea birthday yake ya kutimiza miaka 29, Messi amepoteza mchezo wa fainali kwa mara ya tatu mfululizo baada ya ile ya kombe la dunia dhidi ya Ujerumani mwaka 2024, kisha mwaka uliopita wakafungwa kwenye fainali ya Copa America na wenyeji wa michuano hiyo Chile kabla ya kupoteza fainali ya Copa America ya mwaka huu.

Mchezji huyo bora wa FIFA marea tano ameshinda taji la ligi ya mabingwa Ulaya mara nne na makombe nane ya La Liga akiwa na klabu ya FC Barcelona, lakini hajawahi kutwaa kombe lolote akiwa na timu ya wakubwa ya Argentina.

Wakiadhimisha miaka 100 ya shirikisho la soka la America ya kusini, michuano ya mwaka huu ilikuwa na ongezeko la timu na kufikia mataifa 16 ambayo yalichuana nchini Marekani huku Argentina wakiwa na matumaini makubwa ya kutwaa kombe la michuano mikubwa kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1993.

Kwenye mchezo wa fainali uliokuwa mgumu na upinzani mkali, ulishuhudiwa kila upande ukipoteza mchezaji mmoja kwa kadi nyekundu huku zikitoka jumla ya kadi nane za njano kwenye pambano hilo lililomalizika bila goli ndani ya dakika 90 na kuongezwa nyingine 30.

Messi ambaye amefunga magoli matano kwenye michuano hii, alipiga free-kick ya umbali wa mita 28 baada ya yeye mweyewe kufanyiwa madhambi na Francisco Silva lakini mpira uligonga mabeki na kupita juu kidogo ya mtambaa panya.

Golikipa wa Argentina Sergio Romero alipangua tuta la Arturo Vidal na ikawa zamu ya Messi anayetajwa kuwa mcheaji bora wa kizazi chake huku akifananishwa na mkongwe wa Brazil Pele na Diego Maradona wa Argentina kwa kuwa wachezaji bora wa soka wa muda wote.

Akiwa ameshinda tajia la Olympic akiwa na kikosi cha Argentina cha Under-20, watu wengi wanaamini anahitaji kombe akiwa na timu yake ya taifa kuuhakikishia ulimwengu anaingia kwenye kundi la wachezaji bora wa muda wote duniani.

Nicolas Castillo na Charles Aranguiz wakakwamisha mikwaju yao ya penati kwa upande wa Chile, wakati Javier Mascherano na Aguero nao wakafunga yakwao na kutengeneza sare ya 2-2 baada ya kila upande kupiga penati tatu.

Jean Beausejour akaiweka mbele Chile kisha Bravo akaokoa penati ya Lucas Biglia kisha ikafika zamu ya Silva, kiungo mwenye miaka 30. Messi akajifunika uso kwa jezi yake asione kinachotokea.

Ilikuwa ni fainali ya nne nne kwa Messi kupoteza ambaye alikuwepo pia kwenye kikosi cha Argentina kilichofungwa kwa penati na Brazil kwenye mchezo wa fainali mwaka 2004.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video