Kwenye ratika hiyo, City imepaga kucheza michezo mitatu ugenini, ambapo itaanza kwa kushuka dimbani Kamuzu Stadium jijini Blantyre Juni 18 kucheza na vigogo wa soka nchini Malawi, Big Bullets, ambapo kwa mujibu wa waandaaji, mchezo unatarajia kushuhudiwa na watazamaji wengi hasa ukizingatia ushawishi wa timu hiyo kwenye soka la nchi hiyo.
Mkuu kitengo cha habari na mawasiliano kwenye kikosi cha City, Dismas Ten , amesema kuwa mchezo wa pili nchini humo utachezwa jijini Lilongwe na utakuwa dhidi ya wenyeji Civo United, kwenye dimba la Civo Stadium hii itakuwa ni Juni 21.
“Baada ya mchezo huo wa pili jijini Lilongwe,tutarudi kwenye mji ulio kaskazini mwa nchi hiyo, Mzuzu, hapo tutacheza na wenyeji wetu Mzuni Fc, Juni 25 huu utakuwa mchezo wa mwisho kwenye ziara hii ya michezo ya kirafiki, baada ya hapo tutarudi nyumba tayari kwa michezo mingine ambayo imepangwa ukiwemo dhidi ya Simba tutakaocheza Morogoro”
RATIBA YA MICHEZO YA MATAYARISHO YA MSIMU MPYA IKO HIVI:
- JUNI 18 : Big Bullets Vs City – KAMUZU Stadium. 16:00pm EAT.
- JUNI 21: Civo United Vs City – Civo Stadium. 16:00pm EAT.
- JUNI 25: Mzuni FC Vs City – Mzuzu Stadium. 16:00pm EAT.
- JULAI 31: City Vs Simba Sports- Jamhuri Stadium. 16:00pm EAT.
Kama mambo yatakwenda sawa, ratiba hii inaweza kuwa na ongezeko la michezo miwili ya kirafiki katikati ya mwezi julai kabla ya mchezo wa mwisho wa mwezi huo dhidi ya Simba na mwingine mwanzoni mwa mwezi wa nane kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu.
City inatarajia kuondoka jijini Mbeya Juni 16, kuelekea jijini Blantyre tayari kwa michezo hiyo 3
0 comments:
Post a Comment