Sunday, June 26, 2016

Hatua ya 16 bora ya michunao ya Euro mwaka 2016 inaendelea tena leo, ambapo michezo mitatu tena itapigwa katika viwanja tofauti. Saa kumi za jioni kwa saa za Afrika Mashariki wenyeji wa michuano hii Ufaransa watakuwa wakimenyana na Ireland, Ujerumani na Slovakia watacheza saa moja, wakati mchezo wa mwisho kwa siku ya leo utawakutanisha Hungary na Ubelgiji.
Tukiungazia mchezo kati ya Ufaransa na Ireland ambao utapigwa kunako uwanja wa Stade des Lumieres uliopo manispaa ya jiji la Lyon. Huu ni mchezo ambao unazikutanisha timu mbili zilizofuzu kwa namna tofauti, Ufaransa walifuzu baada ya kumaliza kinara wa kundi A mbele ya timu za Uswisi, Albania na Romania wakati Jamhuri ya Ireland imefuzu kama mshindwa bora (best loser) wa kundi E nyuma ya timu za Italy na Ubelgiji na mbele ya Sweden.
Ufaransa wataingia katika mchezo wa leo wakiwa fiti kabisa baada ya kupata mapumziko marefu zaidi ya wapinzani wao.
Wanatarajia kuwarejesha nyota wake kama vile Dimitri Payet, N'Golo Kante na Blaise Matuidi, ambao walipumzishwa kwenye mchezo uliopita dhidi ya Uswizi.
Olivier Giroud na Adil Rami walikosa mazoezi ya mwisho jana kutokana na kupata maumivu madogo lakini taarifa mpya zinadai watakuwepo katika mchezo huu.
Kwa upande wao Jamhuri ya Ireland, watakuwa na wasiwasi wa kumtumia beki wao Stephen Ward ambaye anasumbuliwa na maulivu ya kifundo cha mguu.
Alifanikiwa kumaliza mchezo dhidi ya Italy ambao waliibuka na ushindi wa bao 1-0, licha ya kuwa na maumivu hayo tangu katika kipindi cha kwanza cha mchezo lakini leo bado hakuna uthibitisho rasmi kama ataanza ama la. 
Mshambulizi Jonathan Walters, ambaye alikosa michezo miwili ya awali kutokana na majeraha ya nyama za mguu, amerudi mazoezini na kuna uwezekano mkubwa akaanza kwenye mchezo wa leo.
Kocha wa Ireland Martin O'Neill amesema mchezo utakuwa mgumu kutokana na ubora wa wapinzani wao ukiongeza na uenyeji wa mashindano, lakini atatumia mbinu ya wachezaji wake kucheza kitimu ili kupata matokeo.
Mshambuliaji Shane Long amesema mchezo utakuwa ni mgumu lakini wenye maana kubwa sana kwao.
"Ni mchezo mgumu, lakini tutautazama kwa namna ambavyo huwa tunafanya katika michezo mingine." alisema.
"Tutafanya kila mbimu kuhakikisha tunawadhibiti kupitia mipira yao ya kutenga (set-pieces), ubora wao kwa mchezaji mmoja mmoja ili kuweza kuwafunga."


Takwimu za mechi walizokutana
  • Ufaransa hawajafungwa kwenye michezo yao mitano ya mwisho dhidi ya Jamhuri ya Ireland (wameshinda, sare mara 3).
  • Mara ya mwisho Ufaransa kufungwa na Jamhuri ya Ireland ilikuwa na katika fainali za Kombe la Dunia mwaka 1981. Walifungwa mabao 3-2 (Ireland walikuwa wenyeji wa fainali hizo).
  • Michezo mitano ya mwisho waliyokutana imetoa magoli manne tu (likiwemo moja la Irend kupitia kwa Robbie Keane kwenye uwanja wa Stade de France).
Ufaransa
  • Mara ya mwisho Ufaransa kumaliza kama vinara wa kundi katika Michuano ya Ulaya ilikuwa ni mwaka 2004, ambapo hata hivyo baadaye walitolewa na Ugiriki katika hatua ya robo fainali.
  • Hawajafungwa kwenye michezo yao 15 ya mwisho katika michuano mbalimbali katika ardhi yao, wameshinda michezo 13 na kutoka sare mara mbili.
  • Mara ya mwisho Ufaransa kushinda mchezo wa hatua ya mtoano katika Michuano ya Ulaya ilikuwa dhidi ya Italy mwaka 200. Tangu hapo hawajawahi tena kufanya hivyo, walipoteza dhidi ya Ugiriki mwaka 2004 na uhispania mwaka 2012.
  • Ufaransa hawajawahi kuruhusu wapinzani wao kupiga shuti lililolenga lango ndani ya dakika 205 katika michuano ya Euro mwaka huu.
  • Magoli tisa kati ya 10 yaliyofungwa na Ufaransa katika michuano ya Ulaya, yamepatikana katika kipindi cha pili
  • Three of their four goals at Euro 2016 have come from the 89th minute onwards.
  • Magoli matatu kati ya manne waliyofunga katika michuano ya Euro mwaka huu, yamepatikana kuanzia dakika ya 89 kuendelea.
Jamhuri ya Ireland
  • Jamhuri ya Ireland wameingia katika hatua ya mtoano kwenye michuano hii kwa mara ya kwanza kabisa katika historia ya taifa lao.
  • Ushindi wao dhidi ya Italy Jumatano iliyopita ulikuwa ni ushindi wao wa pili katika michuano hii na ushindi wao wa kwanza tangu walivyowafunga England mwaka 1988. Ushindo wote huo ulikuwa ni kwa tofauti ya goli moja.
  • Magoli yote ya Jamhuri ya Ireland kwenye michuano ya Euro mwaka huu yamefungwa na wachezaji wa Norwich City.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video