"Sitasahau kipindi chote nilichokuwa na Borussia Dortmund na ningependa kuishukuru klabu na mashabiki kwa sapoti yao kwa kipindi chote cha miaka mitani niliyokuwa klabuni pale".
"Wao ndio walionifunguliwa njia ya kuwa kama nilivyo, na kuwa mchezaji bora kutokana na imani na uvumilivu wao mkubwa kwangu
Sasa naenda kukutana na changamoto mpya ambayo ni kujitolea ili kuleta mafanikio kwa Manchester City. Fursa ya kufanya kazi na kocha aina ya Pep Guardiola ni adhimu mno kwangu, na nimefurahishwa sana kuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa chini yake.
"Nawaahidi mashabiki wa City kujitolea kwa kila kitu kuisaidia timu kushinda mataji mengi hapa England na Ulaya pia (Champions League). Hizi ni nyakati za kuvutia sana.”
"Naamini nina miaka kadhaa ya mafanikio mbele na nadhani tunaweza pia kufanikiwa mambo mengi sana kwa pamoja. Nasubiri kwa hamu kubwa msimu mpya nikiwa katika klabu mpya.
Gundogan ni windo la kwanza la Manchester City kukamilika, wengine wanaowaniwa kwa karibu na City ni beki wa Athletic Bilbao Aymeric Laporte na beki wa Everton John Stones.
Wengine ni kiungi wa Real Madrid Mjerumani Toni Kroos Paul Pogba wa Juventus.
Gundogan anakuwa mchezaji wa pili muhimu Dortmund kuondoka baada ya beki wa kati Mats Hummels kusajiliwa na Bayern Munich.
0 comments:
Post a Comment