Saturday, June 11, 2016

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayecheza soka la kulipwa kunako klabu ya Zesco United ya Zambia, Juma Ndanda Liuzio leo katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Facebook maarufu kama FB ali-post picha ya kiungo wa zamani wa Timu ya Taifa ya soka ya Tanzania,  Taifa Stars, Shaaban Musa Nditi.
Nditi ambaye kwasasa ni mchezaji mwandamizi wa kikosi cha wakata miwa wa Mtibwa Sugar anawavutia wachezaji wengi vijana kwa namna alivyodumu kwenye soka la ushindani.
Pengine kwa wenye kumbukumbu nzuri, Nditi,  ndiye alikuwa kiungo aliyemvutia zaidi kocha wa Taifa Stars kuanzia mwaka 2006-2010, Mbrazil, Marcio Maximo.
MPENJA SPORTS imeamua kumuuliza Liuzio ambaye alicheza na Nditi wakati akiitumikia Mtibwa Sugar kabla ya kutimkia Zambia, kwanini anampenda kiungo huyo Mkongwe?
"Nampenda sana huyo bro. Pia alikuwa ananishauri sana toka nipo Mtibwa hadi  leo. Mimi ni shabiki wake pia.  Napenda anavyocheza mpira". Alijibu Liuzio.
Liuzio, kipenzi cha mashabiki wa Zesco aliendelea kufafanua.
"Nditi mi namkubali sana, hana roho mbaya kabisa ingawa wengi  wanamwogopa kwa jinsi anavyoonekana 'serious',  ila mimi nilikuwa naongea naye vizuri na tunataniana".
Kwasasa Liuzio hajumuishwi kwenye kikosi cha Taifa Stars, huku ukweli ukibaki kuwa yeye ni miongoni mwa wachezaji wachache wa Tanzania wanaocheza kwa kiwango kizuri nje ya nchi.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video