Tuesday, June 14, 2016

Na Hassan Rajabu
Kama tunavyofahamu katika Ulimwengu  huu wa soka kuna vitu vingi vinasababisha timu yoyote kuwa na mafanikio, ikiwemo uongozi bora, uwekezaji na timu bora.
Na leo katika makala yetu tutazungumzia namna klabu ya Yanga inavyoweza kutimiza  ndoto za wanayanga kwa ujumla.

Manji na Ynga ya sasa
Bila shaka tunafahamu namna gani Manji alivyochangia kwa kiasi kikubwa katika mafanikio ya Yanga na kuelekea kuifanya Yanga kuwa 'Yanga ya ndoto za Wanayanga'.
Alianza kama mfadhili na baadaye kugombea nafasi ya uenyekiti na kushinda nafasi hiyo. Hapo ndipo habari mpya zilipoanza kubadilika kutoka  Yanga ya goli tano hadi hatua ya robo fainali katika mashindano ya Kombe la Shirikisho  barani Afrika ambapo wataanza na Mo Bejaia ya Algeria katika michuano hiyo Juampili June 19, mchezo utakaochezwa Algeria.
Pia katika kundi hilo wamo TP mazembe  ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo (DRC)  na Medeama FC ya Ghana,  kwahiyo ni juhudi za Yanga wenyewe kujihakikishia nafasi ya kuendelea mbele katika michuano hiyo.
Ikumbukwe kuwa  terehe June 11 mwaka huu, Yanga walifanya uchaguzi na  Manji kuibuka kidedea baada ya ya kushinda bila kipingamizi.
Ikumbukwe kwamba Manji aliingia madarakani mwaka 2013, baada ya Mwenyekiti  wa wakati huo Lloyd nchunga kujiuzulu baada ya wanachama kumtaka aachie wadhifa huo kutokana na kushindwa kuleta maendeleo  ndani ya klabu hiyo yenye maskani yake mitaa ya  Jangwani.
Katika maana halisi, uongozi wa Yanga chini ya Yusuph Manji,  ndiyo uongozi  bora kutokana na ukweli kwamba katika utawala wake kumetokea vitu vingi kama baadhi ya viongozi  na wanachama kujiuzulu na kufutwa uanachama kutokana na kashfa mbalimbali.
Na vilevile tangu aingie madarakani, Yanga imebadilika na kuwa ya kiushindani zaidi kutokana na kushiriki katika michuano mikubwa kama Klabu Bingwa Afrika na Kombe la Shirikisho mara tatu mtawalia.

Matumizi ya fedha
Katika suala hili wengi tunafahamu ni kwa namna  gani Yanga walivyotumia pesa katika kuiendesha klabu yao ili kuhakikisha inapata mafanikio .
Bila shaka  tunafahamu kuwa tangu Manji aingie madarakani kuna usajili mkubwa sana umefanyika ndani ya klabu na hivyo kuleta mabadiliko ndani ya klabu.
Usajili wa wachezaji kama Thabani Scara kamusoko, Donald Dombo Ngoma, Hassan Ramadhan kessy, Deus kaseke na Amis tambwe na wengine wengi imekuwa ni chachu ya mafanikio kwa klabu hiyo.
Hivyo kusababisha mabadiliko makubwa ndani ya klabu kutokana na usajili huo na uwekezaji wa pesa ndani ya klabu.

Yanga ya ndoto za Wanayanga
Kama tunavyofahamu kuwa mashabiki wa Yanga wana matumaini makubwa  na klabu yao kutokana na mwenendo mzuri  wa klabu, hivyo basi kuamini kuwa wao ni wa levo nyingine ‘’Wakimataifa’’ kwasababu ya ushiriki wao wa mara kwa mara katika michuano ya kimataifa.
Kuna msemo wa wahenga unaosema 'penye nia pana njia' , kwahiyo  Yanga wanatakiwa waamini katika nia waliyonayo na kuna msemo wa wahenga unaosema ‘’mtaka cha uvunguni sharti ainame’’ kwa maana ya kuwa  Yanga inatakiwa kufanya juhudi zozote ili wafike mbali zaidi katika michuano mbalimbali ngazi ya vilabu.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video