Monday, June 13, 2016

Na Hassan Rajabu
Wakati Dunia ikitazama machafuko na kashfa mbalimbali za kisiasa zinazotokea katika Nchi kadhaa katika Dunia hii zikiwemo Brazili , Syria ,Israel na Palestina.
Leo tutazungumzia kuhusu Brazili ya Dilma roussef, Brazili ambayo imekumbwa na kashfa ya rushwa hivi karibuni na Rais akituhumiwa kuhusika na kashfa hiyo.
BRAZIL YA KUIGIZA KATIKA ULIMWENGU WA SOKA.
Ni kama filamu ya kuigiza ambapo tajiri anafilisika na mfanyakazi wake kuwa bosi wake, ni ajabu sana kwa kitu kama hiki na ni aibu pia kwasababu ni fedheha sana kwa bosi kufilisika ,hicho ndicho kimeikumba Brazili ya kizazi hiki cha Dilma roussef  mwenye kashfa za rushwa .
Brazili ya sasa si kama ya zamani,  ile ambayo ilianza kwa kina Garincha,ikaja kwa Pelle, na kumalizikia kwa vizazi vya kina Romario, Rivaldo, Bebeto, Ronaldo de Lima na Ronaldinho ‘Gauncho’.
Brazil hii ilikuwa ni moto wa kuotea mbali kwa kadri vizazi vilivyokuwa vinakuja, walitoka watu wenye vipaji vya ajabu na hivyo kuipa umaarufu timu yao ya Taifa na kutwaa makombe makubwa sana  ulimwenguni huu yakiwemo Kombe la Dunia na Copa America. Brazil wamechukua Kombe la Dunia mara tano (mara nyingi zaidi kuliko taifa lolote duniani), huku Copa America wakiweka kibindoni mara nane, nyuma ya Uruguay (15) na Argentina (14).
Wakati michuano ya Copa America ikifikisha miaka mia tangu kuanzishwa kwake, huku ikendelea kutimua vumbi katika  Nchi ya Marekani katika viwanja mbalimbali, kuna maajabu yaliyojitokeza katika michuano hiyo. Timu kubwa kama Brazili, Uruguay na Colombia zimeshindwa kujihakikishia nafasi ya kuendelea mbele katika michuano hiyo.
Brazili ya kizazi hiki haina maajabu tena imekosa ubunifu,mbinu na morali wa kutafuta matokeo, imekuwa  si ya dhahabu tena wala si lulu tena, imekuwa ni timu ya maigizo.
 Brazili hii imefilisika kisoka inashindwa hata na Peru kwenye michuano ya Copa America ,Brazili hii inatolewa na Peru?,ama kweli mpira unadunda na Dunia inazunguka na hapa ndipo mfanyakazi anapomuajiri bosi wake.
Brazil  hii imebaki jina tu na wachezaji wengi wanalipwa pesa ndefu katika vilabu vyao, hivyo kujikuta wanakuwa mabishoo wasio na ari ya kulitumikia taifa lao.
Wanakosa nuru ya soka katika miguu yao na badala yake wanabaki kuuza  sura zao, hawana tena njaa ya makombe kama vizazi vya Brazili iliyopita wamekosa morali na bashasha katika sura zao na mioyoni mwao  kama kina enzi za kina Ronaldo na Ronaldinho.
Brazil hii itakuwa mwenyeji wa michuano ya Olimpiki, sijui itakuaje? maana ni maajabu yatakayotokea imeshindwa kufanya vema katika michuano ya Copa America ,itakuwa kwenye michuano hiyo? Sijui, ngoja tusubiri maajabu mengine ila isije ikatokea aibu ile ambayo iliwadhalilisha Wabrazil  wote .

NINI KIFANYIKE ILI KUINUSURU BRAZIL  KUTOKANA NA DHAHAMA HILI?
Brazili inatakiwa iwe na morali, njaa na tamaa ya kutwaa makombe katika michuano yoyote itakayoshiriki ili kurudisha heshima ya zamani ya Brazili ile ambayo ilikuwa na njaa ya, morali,na tamaa ya ushindi katika kila michuano iliyokuwa ikishiriki.
Wachezaji wanatakiwa wang’ae katika miguu yao na sio katika sura zao ili kuipa heshima timu yao na kujipa heshima na wao wenyewe kwa kuvaa medali za kimataifa katika timu yao.
Kuna msemo wa wahenga walisema; “usiache mbachao kwa msala upitao” kwa maana kwamba wanatakiwa wajifunze kutoka kwa ‘maveterani’ au wakongwe waliocheza katika timu ya taifa ili wajue namna gani  walikuwa wakipigana na kupambana ili kusaka ushindi kwa udi na uvumba.
Lazima Brazili ibadilike kisaikolojia, lazima wachezaji wakue kiakili [wawe matured] na sio kuwa mabishoo ili kuweza kurudisha heshima ya Brazil ambayo watu walikuwa wakiihusudu.
Ahsante sana ,uwe na siku nzuri msomaji .
  

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video