Monday, June 20, 2016

Mlinzi wa kati wa Simba sc aliyekuwa akicheza kwa mkopo katika klabu ya Coastal Union iliyoshuka daraja mwishoni mwa Msimu uliopita, Miraji Adam 'Mr Freekick' leo kwenye akaunti yake ya facebook, ame-posti picha zake wakati alipokuwa anakipiga na wagosi hao wa kaya na kuweka maneno yanayosomeka -Acha ibaki stori....!!!?
Kitendo hicho kimezua maswali kwa mashabiki wake wakitaka kujua anamaanisha nini?
MPENJA SPORTS imemtafuta Miraji na kumuuliza maana ya post yake ya leo.
" Nimepost tu kwa kuikumbuka timu yangu ya Coastal, daaah! Isingeshuka daraja ningeendelea kubaki pale, lakini ndio basi...imebaki stori. Coastal niliishi vizuri sana, wee acha kabisa'. Amejibu Miraji.
Pia nyota huyo ambaye bado Simba hawajamuongezea mkataba mwingine kwasababu wa sasa unaisha mwezi Julai mwaka huu, amesema baadhi ya viongozi wa Simba walishamwambia atarudi, lakini kwasasa wamekaa kimya.
"Mkataba wangu unaisha mwezi wa saba, nilishaongea na Simba kwamba sitasajili sehemu nyingine kwasababu walisema wataniongeza mkataba, lakini mpaka sasa wamekaa kimya na Mimi nilishapanga muda wangu, ukiisha, nasaini timu nyingine. Kuna timu nyingi zinanihitaji". Alisema Miraji.
Simba inaendelea na Usajili wake na tayari katika nafasi ya ulinzi walishamsaini Emmanuel Simwanza wa Mwadui ambaye kiuchezaji hakumfikia Miraji Adam aliyekuwa na mchango mkubwa kwa Coostal Union.
Wachezaji wengine walionaswa na Simba ni Jamal Mnyate (Mwadui), Mzamiru Yassin (Mtibwa Sugar) na Mohamed Ibrahim (Mtibwa Sugar), huku taarifa za uhakika zikisema wapo mbioni kumalizana na aliyekuwa beki wa Julia wa Coastal Union, Hamad Juma.
Juma anatarajiwa kurithi nafasi ya Hassan Kessy aliyetimkia Yanga, huku Emely Nimuboma akiwa hatarini kuachwa

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video