Wachezaji wa Yanga, kutoka kushoto ni Hassan Kessy, Nadir Cannavaro, Saimon Msuva na Juma Mahadhi wakiajiandaa kukwea pipa kuelekea Uturuki ambapo timu yao itaweka kambi kwa ajili ya kukabiliana na MO Bejaia, katika mchezo wa kwanza hatua ya makundi Kombe la Shirikisho utakaopigwa nchini Algeria June 19.
Kessy na Mahadhi wamesajiliwa kuongeza nguvu katika kikosi hicho baada ya taratibu za CAF kuruhusu klabu kuongeza wachezaji watatu pale inapofika hatua ya nane bora.
Hii inakuwa ni mara ya kwanza kwa wanandinga hao kushiriki katika michezo ya kimataifa baada ya kushindwa kufanya hivyo wakiwa na klabu zao.
0 comments:
Post a Comment