Wednesday, June 8, 2016

Leo familia nzima ya soka barani Afrika imempoteza mtu muhimu sana aliyekuwa na mchango mkubwa katika soka la Afrika. Huyu si mwingine bali ni Stephen Keshi, kocha mzawa wa Nigeria mwenye historia ya aina yake katika soka la Afrika.
Mapema leo asubuhi vyombo mbalimbali nchini Nigeria vimeripoti kuwa Keshi amefariki kutokana na maradhi ya shambulio la moyo. Umati huo umemkuta huko nchini Benin katika mji wa Edo State.

Stephen Keshi ni nani?.
Stephen Okechukwu Keshi alizaliwa Januari 23 mwaka 1962 huko Azare, Bauchi State nchini Nigeria. Aliitumikia Nigeria kama beki wa kati kuanzia mwaka 1981 mapaka 1995 na baadaye kuwa kocha wa taifa hilo. Baada ya muda wake mwingi katika maisha yake ya soka ngazi ya klabu kuutumia akiwa Ubelgiji, Keshi aliamua kwenda nchini Marekani kwa ajili ya mafunzo ya ukocha.
Amewahi kucheka katika timu za Lokeren, Anderlecht, RC Strasbourg, RWDM, CCV Hydra, Sacramento, Scorpions na Perlis FA. Maisha yake mengi ngazi ya klabu alicheza kunako klabu ya Anderlecht ya Ubegiji. 
 Alikuwa kocha wa kwanza mzawa kuipa Nigeria kombe la Afrika na wa pili kutwaa kombe la Afrika akiwa kama kocha na mchezaji pia. Wa kwanza kufanya hivyo alikuwa ni Mahmoud El-Gohary wa Misri mwaka 1998.
Akiwa kama mchezaji, Super Eagles ilitwaa ubingwa kwa kuilaza Zambia mabao 2-1,mjini Tunis.
Aliifundisha timu ya taifa ya vijana ya Nigeria mwaka 2001 katika michuano ya vijana Afrika, vile vile kufuzu kwenye michuano ya Kombe la Dunia kwa vijana mwaka 2001 lakini hata hivyo hakufanikiwa kufuzu.
 Baada ya hapo mwaka 2004 mpaka 2006, aliteuliwa kuwa kocha wa timu ya taifa ya Togo, na kufanikiwa kuipeleka kombe la dunia mwaka 2006 kwa mara ya kwanza kabisa. Lakini hata hivyo alitimuliwa kabla ya michuano hiyo kuanza na nafasi yake kuchukuliwa na Mjerumani Otto Pfister baada ya Togo kuhindwa kufuzu kucheza michuno ya Afrika mwaka 2006 yaliyofanyika nchini Misri.
Amewahi pia kuifundisha Mali baada ya kuteuliwa April 2008 kwa mkataba wa miaka miwili. Hata hivyo alitimuliwa mwaka 2010 baada ya timu hiyo kufanya vibaya katika hatua ya makundi kuelekea kufuzu michuano ya Afrika. 
Keshi aliteuliwa rasmi kuwa kocha wa timu ya taifa ya Nigeria mwaka 2011. Aliiongoza timu hiyo kufuzu michuano ya Afrika mwaka 2013 na kuchukua taji baada ya kuwafunga Burikina Faso kwa bao 1-0. Punde tu baada ya michuano hiyo Keshi alijiuzulu kutokana na hali ya Sintofahamu lakini hata hivyo baadaye walimrejesha. Aliiongiza tena Nigeria katika Michuano ya Kombe la Shirikisho mwaka 2013. Alipata ushindi wa 6-1 dhidi ya Tahiti, akapoteza 2-1 dhidi ya Uruguay kabla ya kufungwa tena na Uhispania mabao 3-0 na kutupwa nje.
Novemba 16 mwaka 2013, Keshi alifanikiwa kuipeleka Nigria kombe la dunia baada ya kuiondosha Ethiopia kwa wastani wa mabao 4-1 kwenye play-off.
On 18 November 2013, Stephen keshi set a record in African football by being the first African coach to successfully qualify two African nations (Nigeria and Togo) to the World Cup Finals. He also helped Nigeria become the first country to achieve an African Cup of Nations trophy and World noshaCup qualification, both in 2013.
Novemba 18 mwaka 2013, Keshi aliweka rekodi katika soka la Afrika baada ya kuwa kocha pekee wa kiafrika kufanikiwa kuzipekeka timu mbili za Afrika Kombe la Dunia ambazo ni Nigeria na Togo. Aliisaidia Nigeria kutwaa ubingwa wa Afrika na kufuzu michuano ya Kombe la Dunia.
Alifanikiwa kuipeleka Nigera hatua ya mtoano kwenye Kombe la Dunia mwaka 2014 ambapo walitolewa na Ufaransa baada ya kufungwa mabao 2-0. Katika hatua ya makundi walitoka suluhu dhidi ya Iran, kushinda 1-0 dhidi ya Bosnia na Herzegovina na kufungwa 3-1 dhidi ya Argentina. Baada ya michuano hiyo Keshi alitangaza kujiuzulu.
Baadaye alirudishwa tena na kupewa mkataba mpya.  Oktoba 14 mwak 2014, Keshi alishindwa kabisa kuipa matokeo mazuri Nigeria baada ya kushindwa kupata ushindi hata katika mechi moja kuelekea kufuzu michuano ya Afrika Morocco mwaka 2015. Baada ya matokeo hayo mabovu alitishia kujiuzulu endapo wangeendelea kumpa mashinikizo kutoka kwa watu ambao aliwashutumu kuwa wanamhujumu. Baadaye tena alitulia na kusema ataendelea kuifundisha timu hiyo kwasababu analipenda taifa lake.
Keshi aliachana na Nigeria July mwaka 2015 baada ya mkataba wake kuisha na waajiri wake (NFF) kutokuwa na mpango wa kumpa mkataba mpya. Hiyo ilitokana na hali ya sintofahamu ilikuwa ikiendelea kuwepo kati ya kocha huyo na waajiri wake.
Baada ya hapo Keshi aliamua kupumzika na kufanya na kufanya shughuli nyingine huku akiwa karibu zaidi na familia yake. Mwaka jana alifiwa na mkewe ambaye amedumu naye kwa takriban miaka 33. Mkewe alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya kansa.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video