Monday, June 13, 2016

Moja ya wachezaji wa kigeni wanaotumia juhudi kubwa kujifunza lugha ya Kiswahili, basi Thabani Kamusoko inawezekana anashika namba moja. Kamusoko kupitia akaunti yake ya Facebook licha ya mara kadhaa kukosea japo kwa uchache baadhi ya herufi, lakini amekuwa akijitahidi kuandika kwa lugha ya kiswahili ili kujaribu kuwasiliana kiurahisi zaidi na mashabiki wa timu yake ya Yanga.
Lakini hii imekuwa tofauti kidogo kwa Mzimbabwe mwenzake Donald Ngoma ambaye hajawahi hata siku moja kuandika neno lolote la Kiswahili.....Pengine inawezekana hajavutiwa na lugha hii.
Hongera Kamusoko juhudi zako zitakufanya ukifahamu Kiswahili mapema zaidi.
Jana kupitia akaunti yake aliandika hivi..."I respect football because it has taken me far ....Mpila nau heshimu sana...⚽⚽".
Licha ya kwamba alitakiwa kuandika mpira nauheshimu badala ya mpila nau heshimu lakini hata hivyo amejitahidi kwa kiasi kikubwa na juhudi zake zinaonekana.


0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video