Saturday, June 4, 2016

THABAN Kamusoko aliyetokea kuwateka vilivyo mashabiki wa Yanga kutokana na soka lake maridadi, amesema kuwa iwapo siku moja atapata fursa ya kucheza timu moja na kiungo wa Simba, Justice Majabvi, basi kikosi chao hicho kitakuwa ni moto wa kuotea mbali kwa wapinzani wao.

Kamusoko amelipasha BINGWA akiwa kwao Zimbabwe kwa ajili ya mapumziko baada ya kumalizika kwa Ligi Kuu Tanzania Bara, akiwa ametoa mchango mkubwa kwa timu yake hiyo kutetea ubingwa wake, lakini pia kutinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Akizungumza kutoka Zimbabwe, Kamusoko alisema kuwa amekuwa akimkubali mno Majabvi, akimwagia sifa hadi kwa lugha ya kikwao akisema: “Hooo saka atotorwa here…iya mdara.” akiwa na maana Majabvi ni mchezaji mzuri sana.

Alipoulizwa iwapo anaweza kuisaidia Yanga kumsajili mchezaji huyo ambaye naye yupo mapumzikoni Zimbabwe, alisema kuwa anaamini iwapo viongozi wake watafunga safari kumfuata kiungo huyo huko kwao, wanaweza kumalizana naye.

Majabvi kwa sasa yupo Zimbabwe ambapo imeelezwa kuwa uwezekano wa kurejea Simba ni mdogo kutokana na masharti aliyowapa Wekundu wa Msimbazi hao ambayo ni kupewa nyumba yenye hadhi yake pamoja na kusomeshewa mwanaye katika shule ya kimataifa, jambo ambalo huenda likiwa rahisi mno kwa Yanga iwapo watamtaka.

Na kwa jinsi Kamusoko alivyomwagia sifa Majabvi, ni wazi kuwa iwapo matajiri wa Yanga watafunga safari hadi Zimbabwe, anaweza kuwasaidia kumshawishi ‘mido’ huyo na hivyo kumaliza tatizo la kiungo mkabaji linaloiandama timu yao hiyo.

Majabvi ameonyesha umahiri wa hali ya juu katika nafasi ya kiungo mkabaji, kiasi cha kutokea kuwa kipenzi cha Wana-Msimbazi, lakini ikielezwa kuwa alisaini mkataba wa mwaka mmoja uliofikia tamati mwishoni mwa msimu huu, japo viongozi wa Simba wamekuwa wakitamba bado ana mkataba wa mwaka mmoja zaidi.

Katika kikosi cha Yanga, hakuna kiungo wa uhakika wa nafasi ya ukabaji ambapo amekuwa akitumiwa Mbuyu Twite na Pato Ngonyani ambao hata hivyo viwango vyao vimekuwa vikitiliwa shaka.

Kwa nyakati fulani, nafasi hiyo wamekuwa wakipangwa Salum Telela au Kamusoko ambao kiasili ni viungo wachezejishaji.

Iwapo Yanga watafanikiwa kumsajili Majabvi, watalazimika kumtema Twite akiwa ni mchezaji wa kigeni kwani tayari imeelezwa kuwa mchezaji wao mwingine wa kigeni, Issoufou Boubacar wa Niger anafungashwa virago.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video