ItaIy wamefuzu hatua ya 16 bora ya michuano ya Euro baada ya kuwafunga Sweden kwa bao 1-0 lililofungwa na Eder Martins dakika ya 88 baada ya kazi nzuri iliyofanywa na Zaza. Mchezo huo ulifanyika kunako dimba la Stade de Tolouse.
Licha ya muda mwingi kutawala mchezo, Sweden kwa mara nyingine leo wameshindwa kupiga hata shuti moja lililolenga lango huku nahodha na mshambuliaji wao Zlatan Ibrahimovic akiwekwa chini ya ulinzi mkali wakati wote wa mchezo.
Italy wanakuwa kileleni mwaka kundi wakiwa na alama sita wakati Sweden wakiwa nafasi ya tatu.
Dondoo muhimu za kufahamu.
- Kulikuwa na wachezaji watatu walioanza kwenye mchezao wa leo ambao pia walianza wakati timu hizi zilipokutana mara ya mwisho mwaka 2004; Buffon kwa upande wa Italy, Isaksson na Ibrahimovic kwa upande wa Sweden (Kallstrom ameanza mchezo wa leo lakini mwaka 2004 aliingia akitokea bechi).
- Goli alilofunga Eder leo lilitokana na shuti lake la kwanza lililolenga lango kwenye michuano hii ya 2016
- Goli la Italy lililofungwa la Italy lilikuwa limetokana na shuti la kwanza lililolenga lango katika kipindi cha pili.
- Sweden ndio timu ya kwanza kucheza mechi zake zote mbili za michuano hii bila kupiga shuti lolote lililolenga lango la timu pinzani. Mara ya mwisho ilitokea mwaka 1980
- Mchezo huu ulikuwa na jumla ya mashuti 12, machache zaidi katika mchezo mmoja kwenye michuano hii tangu mwaka 1980
- Italy bado hawajaruhusu goli lolote mpaka sasa, wamepata clean sheets kwenye michezo yao sita ya mwisho ya michuano ya Euro.
- Kumekuwa na magoli mengi yanayofungwa ndani ya dakika tano za mwisho katika michuano hii (magoli 11) kuliko yaliyopatika katika kipindi cha kwanza (magoli 10)
- Wachezaji sita wamekuwa wakihusika katika magoli matatu ya Italy yaliyopatikana kwenye mechi mbili zilizopita (magoli kutoka kwa Giaccherini, Pelle na Eder na assist kutoka kwa Candreva, Bonucci na Zaza).
0 comments:
Post a Comment