England ina rundo la wachezaji ambao wana asili ya mataifa mengine.
Wakati Uingereza ikijiandaa kufanya marekenisho juu ya sheria zao za masuala ya uhamiaji miaka kadhaa baadaye, England na Wales wapo kweye michunao ya Euro wakiwa na vikosi vyenye muonekano tofauti kabisa.
Nasema mwonekano tofauti kwasababu zaidi ya nusu ya wachezaji waliochaguliwa na makocha Roy Hodgson England na Chris Coleman wa Wales kwa ajili ya michunao ya Euro mwaka huu wana asili kutoka mataifa tofauti tofauti.
Wachezaji 15 wa kikosi cha Ufaransa wana asili kutoka mataifa tofauti.
Kimsingi, hii itakuwa ni michuno ya kipekee tangu kuanzishwa kwake. Idadi ya wachezaji 166 kati ya 552 ambao wamechaguliwa na mataifa yao kwa ajili ya michuano hiyo wana asili ya mataifa tofauti.
Wenyeji Ufaransa ndio wanaongoza kuwa na idadi ya wachezaji wengi wenye asili ya mataifa tofauti, wakiwa na wachezaji 15 kati ya 23 waliochaguliwa kwenye michuano hiyo. Wengi wao ni wale ambao wazazi wao walihama kutoka mataifa ya Afrika kwenda Ulaya hasa Ufaransa. Ukweli huu unachagizwa na maneno ya utani yaliyotolewa na Eric Cantona wiki iliyopita kwamba Benzema, Ben Arfa na Nasri wameachwa kwasababu ya kuwa na asili ya Afrika, jambo ambalo Bacary Sagna alilipinga vikali na kuita suala la 'kipumbavu'.
Switzerland na Albania ziafuatia kwa karibu, zikiwa na wachezaji 14 na 13 mtawalia, ambao wangeweza kucheza katika mataifa mengine kutokana na kuwa na asili ya mataifa husika .
Nyota mya wa Arsenal Granit Xhaka atakuwa akipambana kaka yake Taulant. Wawili hao wana asili ya Albania lakini Granit amechagua kuchezea Uswizi wakati Taulant amebaki Albania.
Kitu cha kuvutia zaidi ni katika mchezo kati ya Albania na Uswizi. Timu zote zina wachezaji ambao wangeweza kucheza kati ya hayo mataifa mawili. Albania wangeweza kuwatumia wachezaji sita wa Uswizi ambao asili yao ni Albania akiwepo Granit Xhaka
Hii inakuwa ni mara ya kwanza kutokea Ulaya ndugu wawili wa damu wakikutana katika mataifa tofauti. Hii ilitokea kwa Jerome na Kevin-Prince kwenye michunano ya Kombe la Dunia mwaka 2014 nchini Brazil, lakini Kevin alikuwa akicheza Ghana ambayo ipo Afrika.
Kwa upande wa England, wao idadi ya wachezaji 12 wana asili ya mataifa mengine, wakiwemo wenye asili ya Kamaica ambao ni Raheem Sterling, Daniel Sturridge, Chris Smalling, Danny Rose na Kyle Walker, Nathaniel Clyne kutoka Grenada, Adam Lallana (Uhispania), na wawili kutoka Nigeria (Dele Alli and Ross Barkley).
Mataifa mengine ni Wales na Jamhuri ya Ireland ambayo kila moja lina wachezaji kumi,wakati Ireland Kaskazini wanao sita.
Chini kabisa, Romania ndiyo taifa pekee ambalo wachezaji wake wote wana asili ya taifa hilo, wakati Iceland, Czech Republic na Slovakia kila moja likiwa na mchezaji mmoja ambaye ana asili ya taifa tofauti.
0 comments:
Post a Comment