Tuesday, June 21, 2016

Katika mchezo wa soka, kama kuna eneo linalotakiwa kuwa la kwanza kutupiwa macho kwa umakini basi ni safu ya ulinzi. Kama timu ina udhaifu mkubwa katika safu ya ulinzi, basi ama hakika haiwezi kuwa na matokeo chanya kwa nyakati nyingi.
Hilo ndilo suala ambalo limekuwa likipewa kipaumbele kwa taifa la Italy kwa miaka neda-rudi. Italy wamekuwa na safu bora ya ulinzi tangu enzi za Franco Baresi, Fabio Cannavaro. Alessandro Nesta, Paolo Maldini.
Kwenye kila mashindano ambayo Italy mara zote amekuwa akishiriki unaweza kudhani kama hawapo vile kutokana na namna wanavyo-approach mechi zao, lakini wakiwa na lengo maalum.
Utashangaa tu wamefika nusu fainali, na hii si kwa kubahatisha ila kwa sababu ya ubora wa soka lao la nidhamu na juhudi ya hali ya juu .
Ukiwatizama wakicheza unatakiwa uwe umetuliza akili na kuwa na umakini mkubwa sana sababu wanacheza mpira wa akili,wanakaba kwa mbinu,wanashambulia kwa mipango na mwisho wa siku huchukua pointi kwa kwa ubora wa hali ya juu na kuondoka wakiwaacha wapinzani wao hawaamini matokeo.
Leo tunaiona Italy nyingine ya Antonia Conte ikiwa na 'instincts' zile zile licha ya kutokuwa na wachezaji wenye hadhi kama  Fillipo Inzaghi ama Christian Vieri, lakini wamebaki na falsafa yao ya kuwa na ukuta imara ambao unasaidia kutoruhusu magoli ovyo, wakati huo huo waishambulia kwa akili ya hali ya juu.
Tumeingalia Italy kwenye michezo miwili iliyopita dhidi ya Ubelgiji na Sweden na kuona jinsi wapinzani wao walivyokuwa wakitawala mchezo lakini mwisho wa siku kuambulia kichapo.
Ukuta wenye nidhamu bora unaoundwa na utatu mtakatifu wa Juventus Andrea Barzagli, Leonardo Bonucci na Giorgio Chiellini umekuwa ni msaada mkubwa kwa matokeo chanya ya Italy katika michezo yote miwili.
Tumeshuhudia katika mchezo dhidi ya Sweden Giorgio Chiellini aliibuka mchezaji bora wa mechi baada ya kumkaba vilivyo Zlatan na kutopiga hata shuti moja langoni mwa Italy.
Licha ya kutokuwepo kwa viungo maridadi kama Claudio Marchisio na Marco Veratti ambao wamekosekana kutokana na majeraha lakini bado Antonio Conte ameweza kutafuta mbinu mbadala ya kuilinda 'back four' yake. Anafanyaje sasa Conte kuwaua wapinzani wake? Kuwakaba timu pinzani kwenye eneo lao wenyewe na kuchukua mipira huko huko na kuwashambulia kwa kasi.

Huu mfumo unafanyaje kazi?
Licha ya sasa kutokuwa na washambuliaji mahiri aina ya Roberto Baggio, lakini Italy bado wameendelea kuutumia mfumo wa 4-2-3-1 ambao ndiyo unawapa matokeo licha ya kuwa ndio mfumo ambao timu nyingi zinafeli kuutumia kwa sasa. 
Conte ameamua kubaki na mfumo huu, huku akiutumia na kuuamini vilivyo ukuta unaoundwa na visiki vitatu vya Jeventus Barzagli, Bonucci na Chiellini ambao kwenye klabu yao mpaka msimu unaisha waliruhusu mabao 20 tu kutikisa nyavu zao, huku wakiongozwa na mkongwe Gianluigi 'Gigi' Buffon.
Wakiwa na wanamiliki mpira, wanapasiana mpira taratibu mpaka wakihakikisha wako salama katika eneo lao. Ikitokea hivyo sasa moja kati ya mabeki wao wa kati ama Barzagli, Bonucci au Chiellini anapanda juu kuungana na Montolivo katika eneo la kiungo.

Wakati huo wachezaji wengi wakiwa katika eneo la timu pinzani, Italy waapeleka mipira katika winga zao kwa kutumia counter-attack na kupiga krosi kwenda katikati ya eneo la hatari la timu pinzani na washambuliaji wao kama Graziano Pellè na Éder Citadin Martins kutumia kichwa kujaribu kufunga kutokana uwepo safu ya timu pinzani kutokuwa imejipanga vizuri kutona na uwepo wa shambulizi la kushtukiza.
Na endapo inatokea wameukosa, basi viungo wao bado wanakuwepo ili kutoa msaada kama kunakuwa na re-bound.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video