Thursday, June 2, 2016

 Naweza kusema vita ama uhasimu unarejea kwa mara nyingine na kunogesha EPL. Tena sio vita vya kawaida maana itakuwa ni vita vya makocha wawili mahasimu na vilabu viwili hasimu. Guardiola atakuwa akiinoa Manchester City msimu ujao wa ligi wakati Jose Mourinho atakuwa akiinoa Manchester United baada ya kumalizana nao kila kitu na kusaini mkataba.
Ikumbukwe kwamba, Guardiola na Mourinho wamewahi kufanya kazi pamoja kwa takriban miaka minne wakiwa ndani ya klabu ya FC Barcelona. Wakati huo Guardiola akiwa kama mchezaji na Mourinho akiwa kama kocha msaidizi wa Bobby Robson na baadaye Louis van Gaal.
Miaka mingi imeshapita na mengi yametokea. Van Gaal akiwa ameshaondoshwa United na kiti chake kuchukuliwa na Mourinho huku Pellegrini akimaliza muda wake na nafasi yake kuchukuliwa na Pep.
Pep Guradiola (kushoto) akibadillisha mawazo na Jose Mournho wakati wawili hao wakiwa pamoja Barcelona.
Tukirudi miaka mingi nyuma kunako klabu ya Barcelona, Pep na Jose walikuwa na maswahiba wakubwa. Guardiola, wakati huo akiwa mchezaji alikuwa akiandaliwa kuwa kocha kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuusoma mchezo uwanjani. Wakati huo huo Guardiola naye alikuwa akimkubali Mourinho kutokana na uwezo wake mkubwa kuelezea mchezo namna unavyokwenda. Walikuwa wakitumia muda mwingi mazoezini kukaa pamoja na kuongelea mbinu mbalimbali za kimchezo.
Wakati Frank Rijkaard akiondoka Barcelona mwaka 2008, Mourinho alikuwa na matumaini makubwa ya kupewa timu. Wakati akiwasilisha mikakati yake mbele ya maafisa wa klabu ya Barcelona katika kikao kilichofanyika Lisbon, Ureno, Mourinho alimwaga sifa nyingi kwa makamu wa rais wa zamani wa klabu hiyo Marc Ingla na kumtaja Guardiola kama kocha msaidizi kama angepewa mikoba ya kuwanoa wakati hao wa Catalunya.
Lakini wakati huo, viongozi wa Barcelona tayari walikuwa na maamuzi kichwani mwao. Mkurugenzi wa Michezo wa Barca wakati huo Txiki Begiristain alipenda Pep ndiyo akabidhiwe timu hiyo kutokana na kufanya vyema akiwa na timu B na hatimaye kukabidhiwa timu hiyo. Sasa suala hilo lilimkera sana Mourinho.
Pep alianza kampeni ya kuionoa Barcelona rasmi msimu wa 2008-09 na kuchukua makombe matatu kwenye msimu wa . Na katika msimu wake wa pili sasa akakutana na Mourinho katika Champions League hatua ya nusu fainali na hatimaye Mourinho kuibuka na kicheko mwishoni baada ya kumtupa Pep nje ya michuano.
Mourinho aliwakasirisha sana mashaniki wa Barca na baadhi ya wachezaji akiwemo  baada ya kusherehekea kwa kukera katika dimba la Camp Nou. Kabla ya mchezo huo Guardiola alizungumza kauli fulani ambayo ilikuwa na mshangao ndani yake, alisema hivi: Sikujua kama Mourinho angefika mbali kiasi hiki, kama ningejua ana kipaji kiasi hiki, ningemwambia rais kipindi kile".
Akiwa na Inter, Mourinho pia alimfunga Van Gaal katika fainali mwaka huo huo, mchezo uliopigwa katika dimba la Santiago Berabeu. Baada ya mechi hiyo alitangaza kuachana na Inter, na hatimaye akatua kunako klabu ya Real Madrid. 
Na ndipo vita yao ikiaanzia kunoga hapo, mchezo wa kwanza wa El Classico, Real Madrid ikiwa chini ya Mourinho ilipokea kipigo kitakatifu cha mabao 5-0 katika dimba la Camp Nou kutoka kwa Barcelona ya Pep Guardiola. 
Baadaye wakakutana tena kwenye La Liga na kutoa sare ya bao 1-1 mchezo uliopigwa Santiago Bernabeu April 16, siku nne baadaye wakakutana katika fainali ya Copa del Rey katika dimba la Mestalla na Madrid wakashinda kwa bao 1-0 lilofungwa na Cristiano Ronaldo baada ya kupata krosi maridhwa na Angel Di Maria.
Baada ya mchezo huo, Guardiola alitupa lawama zake kwa mwamuzi na kusema kuwa: "Mwamuzi msaidizi lazima atakuwa na jicho la aina yake ili kutambua kwamba Pedro alikuwa amezidi kwa sentimita mbili". Alisema hayo kutokana na goli lao lililofungwa na Pedro kukataliwa.
Siku sita baadaye, kuelekea mchezo wa raundi ya kwanza ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa katika dimba la Bernabeu, Mourinho alitoa 'vimaneno' vya kejeli kwenda kwa mpinzani wake.
Alianza kwa kusema hivi:"Tumenza upya , mpaka sasa kuna kundi la makocha wachache sana ambao hawazunguma kuhusu waamuzi na kundi kubwa ambalo na mimi nipo wameshafanya hivyo. Sasa basi, kutokana na comments za pep, tumeingia katika kipindi kipya na kundi jingine la tatu, ambayo yuko peke yake, kundi ambalo linamkosoa mwamuzi kwa kufanya maamuzi sahihi . Hili ni jambo jipya kabisa kwangu".
Kwa upande wake Guardiola alijibu kwa namna hii: Mourinho amechagua kuniita Pep, sasa na mimi namuita Jose". Pep akaendelea kusema: Jose ipi hapa ni camera yako?zote si ndiyo, sasa nasema hivi, kesho saa 8.45 tutaonana uwanjani. Nje ya uwanja amekuwa mshindi mara nyingi, kama anataka kombe lake mwenyewe la Champions League nje ya uwanja, basi acha achukue na aende nalo nyumbani kusherehekea.
Katika ukumbi huu, Mourinho ni kocha mpuuzi. Mwenyewe analitambua vizuri hili na sitaki kushindana naye hapa. Ningependa kumkumbusha tu kamba nilifanya naye kazi kwa miaka minne nikiwa Barcelona kama mchezaji. Ananijua vizuri nami namjua pia.
Kama anapendelea kuchukua mawazo ya waandishi marafiki zake ambao wanamezesha sumu na Florentino Perez na kushindwa kuheshimu uhusiano wetu mzuri tuliokuwa nao kwa miaka minne, basi hilo ni chaguo lake. Najitahidi kujifunza mengi kutoka kwa Jose uwanjani, lakini najitahidi kujifunza machache mno kutoka kwake nje ya uwanja".
Wakati akirejea hotelini kupata chakula, wachezaji wote wa Barcelona walisimama kumsalimia Pep na kumpigia makofi. Kilichotokea uwanjani baadaye Barca waliinyuka Madrid 20- na kumwacha Mourinho akiwalalamikia na kuwatuhumu waamuzi kuihujumu timu yake.
Msimu uliofuata, Mourinho alichukua La Liga akijinasibu kama kocha ambaye amechukua ubingwa huku akiwa amemfunga Guardiola. Na Guardila akaachana na Barcelona kuamua kuchukua mapumziko ya mwaka mzima mwishoni mwa msimu wa 2011-12.
Wawili hao wakakutana tena wakati Pep akiifundisha Bayern na Mourinho akiifundisha Chelsea. Ulikuwa ni mchezo wa UEFA Super Cup na Bayern waliibuka washindi kwa matuta. Tangu hapo wawili hao hawajawahi kukutana tena na sasa wanatarajia kukutana tena katika kivumbi cha EPL msimu ujao wakiwa katika jiji moja la Manchester. Guardiola akiwa na Manchester City wakati Mourinho akiwa na Manchester United. Kazi itakuwepo msimu ujao.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video