Monday, June 20, 2016

England na Slovakia wanaingia uwanjani kusaka tiketi ya kucheza hatua ya 16 bora, mchezo wa kundi B utakaofanyika majira ya saa nne usiku kunako dimba la Stade Geoffroy-Guichard lililopo manispaa ya Saint-Étienne.
Timu zote mbili zinaingia uwanjani zikiwa na lengo la kutafuta ushindi ili kujiwekea mazingira ya kufuzu moja kwa moja kwenda 16 bora.
England wanaingia uwanjani wakiwa na kumbukumbu ya ushindi katika mchezo wa pili dhidi ya ndugu zao wa Wales. Walianza na sare ya 1-1 dhidi ya Russia katika mchezo wa kwanza ambapo katika mchezo huo walipoteza nafasi nyingi za wazi.
Katika mchezo dhidi ya Wales, ilikuwa almanusra wapate sare mpaka pale Daniel Sturridge alipofunga goli la ushindi katika dakika za lala salama. Mabadiliko ya kocha Roy Hodgson kuwatoa Raheem Sterling na Harry Kane na kuwaingiza Jamie Vardy na Daniel Sturridge mtawalia yalitosha kuipa ushindi England kutokana na uhalisia kwamba wachezaji hao ndio waliyofunga magoli baada ya kuingia.
Mpaka sasa kwenye msimamo wa kundi hili, England wanaongoza wakiwa na alama 4, mbele ya Wales na Slovakia wenye alama 3.
Hivyo basi sare yoyote kwa England inampeleka hatua ya mtoano, wakati kwa upande wa Slovakia ni lazima wapate ushindi ili kupata nafasi hiyo.

Taarifa za kila timu.
Roy Hodgson amethibitisha kwamba atawapumzisha wachezaji sita akiwemo Rooney, ambaye alianza kwenye michezo yote miwili iliyopita.

Harry Kane na Raheem Sterling hawakucheza katika kiwango bora katika michezo miwili ya awali na hivyo nafasi zao zitachukuliwa na  Jamie Vardy na Daniel Sturridge ambao wameonesha kiwango bora.

Jordan Henderson na Jack Wilshere ataaanza kwa mara yake ya kwanza katika mchezo wa leo kuchukua nafasi za Dele Alli na Wayne Rooney huku mfumo pia ukibadilika na kutumia 4-3-3.

Mabeki wawili wa Tottenham Kyle Walker na Danny Rose watapumzishwa na nafasi zaoo kuchukuliwa na Ryan Bertrand na Nathaniel Clyne.

Licha kukusolewa kutokana na kuruhusu goli la kizembe katika mchezo dhidi ya Wales, Joe Hart bado atabaki kuwa chaguo la kwanza kwa kocha Roy Hodgson na kuanza mchezo wa leo.

Kocha wa Slovakia Norbert Gyombér bado anaingiza kikosi chake kile kile isipokuwa Jan Kozak ambaye kuna wasiwasi wa kutocheza kutokana na kuwa na majeraha, lakini wachezaji wote waliocheza katika mchezo dhidi ya Russia wataanza kwenye mechi ya leo.

Mechi walizokutana
  • Engalnd wameshinda michezo yao yote mitatu iliyopita waliyocheza dhidi ya Slovakia, ikiwemo ile ya kufuzu Euro mwaka 2004.
  • Mara ya mwisho kukutana katika mchezo wa kirafiki, England walishinda mabao 4-0. Rooney alifunga mara mbili katika mchezo huo na kutimiza magoli 20 na 21, kwa sasa na magoli 52.
  • Magoli saba kati ya nane ya Engalnd dhidi ya Slovakia yamefungwa baada ya dakika ya 60.
Slovakia
  • Slovakia hawajapata clean sheet katika michezo yao sita iliyopita katika mashindano yoyote.
  • Marek Hamsik amehusika katika magoli manne kwenye michezo mitatu ya mwisho akiwa na Slovakia (amefunga magoli matatu na kutoa pasi moja ya goli)
  • Mashuti 20 kati ya 22 ya Slovakia kwenye michuano ya Euro mwaka huu yamewahisiha ama Hamsik, Vladimir Weiss au Robert Mak involved.
England
  • Katika uwanja huu wa Geoffroy Guichard, mara ya mwisho England walicheza katika hatua ya 16 bora ya Kombe la Dunia mwaka 1998 dhidi ya Argentina na kutoka sare ya 2-2 na baadaye kufungwa kwa penati 4-3.
  • Mchezo huo ulikuwa maarufu baada ya David Beckham kupata kadi nyekundu kufuatia kumpiga teke Diego Simeone ambaye kwa sasa ni kocha wa Atletico.
  • Ukiondoa mikwaju ya penati, England hawajafungwa katika michezo yao nane ya ya mwisho katika michunao ya Euro (wameshinda mara tano, sare mara nne). Hiyo tangu walivyopoteza dhidi ya Ufaransa kwa magoli 2-1 Euro ya mwaka 2004.
  • Jamie Vardy ndiyo kinara wa ufungaji kwa England kwa mwaka 2016 akifunga magoli 4 katika michezo mitano

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video