England wamemaliza maandalizi yao kwa ajili ya Euro 2016 kwa ushindi mwembamba dhidi ya kikosi cha wachezaji 10 wa Ureno kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliochezwa usiku wa jana kwenye uwanja wa Wembley.
Chris Smalling aliifungia England goli pekee la ushindi akiunganisha kwa kichwa krosi ya Raheem Sterling dakika nne kabla ya pambano kumalizika mchezo ulioshuhudia vijana na Roy Hodgson kuwafunga Ureno waliokuwa pungufu baada ya Bruno Alves kutolewa kwa kadi nyekundu kwa kumchezea vibaya Harry Kane dakika ya 35 kipindi cha kwanza.
Kyle Walker pekee ndiye mchezaji wa England aliyeonesha kiwango cha juu licha ya Sterling kuonesha uwezo wa juu pia alipoingia akitokea benchi.
Kitu pekee kinachompa nguvu Hodgson, ni kumalizika kwa mchezo huo bila wachezaji wake kupata majeraha na sasa mawazo yake yote anayaelekeza kwenye mchezo wake wa kwanza dhidi ya Russia kwenye michuano ya the Euro 2016 unaotarajiwa kuchezwa June 11.
Rekodi mbalimbali zilizowekwa kwenye mchezo wa England vs Ureno.
- Chris Smalling amefunga goli lake la kwanza akiwa timu ya taifa ya England akiwa ameichezea timu hiyo michezo 25 hadi sasa.
- Magoli matatu ya mwisho ya England yamefungwa na wachezaji watatu tofauti kutoka kikosi cha Manchester United (Marcus Rashford, Wayne Rooney pamoja na Chris Smalling).
- Bruno Alves amekuwa mchezaji wa kwanza kutolewa kwa kadi nyekundu kwenye mchezo unaoihusisha England kwenye uwanja wa Wembley tangu Steven Gerrard alipooneshwa kadi nyekundu mwaka 2012 wakati England ikicheza dhidi ya Ukraine.
- England imepata ushindi wa kwanza dhidi ya Ureno tangu April 1998, ikiwa imeshacheza michezo mitano dhidi yao bila kupata ushindi.
- England maarufu kama ‘Three Lions’ wameruhusu kufungwa magoli matatu pekee kwenye mechi zao 11 walizocheza kwenye uwanja wa Wembley.
- Ureno walishindwa kupiga shuti hata moja on target ndani ya dakika zote 90 za mchezo huo.
0 comments:
Post a Comment