England wameruhusu goli la kusawazisha dhidi ya Russia dakika za lala salama kwenye mchezo wa Kundi B kwenye michuano ya Euro 2016 na kushuhudia mechi hiyo ikimalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1.
Kikosi cha Roy Hodgson kilitawala mchezo kwa asilimia nyingi lakini kilipoteza nafasi kadhaa kabla ya kiungo mkabaji Eric Dier kupachika bao la kuongoza kwa mkwaju wa free-kick mita 20 kutoka langoni.
Golikipa wa Russia Igor Akinfeev alifanya kazi ya ziada kuokoa michomo kutoka kwa Adam Lallana na Wayne Rooney ambao mashuti yao yalipanguliwa juu kidogo ya ‘mtambaa panya.
Goli la kichwa kutoka kwa Vasili Berezutski limewaacha England wakiwa hawana la kufanya kutokana na goli hilo kufungwa dakika ya 90 ya mchezo
England wamepoteza nafasi ya kukaa kileleni mwa Kundi B pamoja na wenzao Wales ambao walishinda mchezo wao kwa bao 2-1 dhidi ya Slovania mapema Jumamosi.
Hodgson alimtoa man of the match Wayne Rooney ambaye awali aliachia kiki kali iliyopanguliwa na golikipa wa Russia Akinfeev, nafasi ya Rooney ikachukuliwa na Jack Wilshere.
Sare hiyo imeendeleza rekodi ya England ya kushindwa kupata ushindi kwenye mechi zao za kwanza za michuano ya Ulaya baada ya kubanwa dakika ya pili kati ya nne za mwisho.
Hodgson amei-cost England?
Kocha wa England Roy Hodgson alifanya uchaguzi sahihi wa kuamua kupanga kikosi cha kwanza na kumchezesha Wayne Rooney katika nafasi ya kiungo lakini mabadiliko aliyoyafanya ndiyo kosa kubwa lililobadili mchezo.
Alimpumzisha Rooney mara tu baada ya Dier kufunga goli na nafasi yake kuchukuliwa na Wilshere wakati alikuwa ndiye mchezaji aliyeipa uhai England kwa kiasi kikubwa. Rooney mwenye miaka 30 alionesha kiwango kizuri na kuonekana kama bado kijana kwa namna alivyopambana.
England ingekuwa na nguvu ya kumaliza mchezo ikiwa na ushindi mbele ya Russia lakini mabadiliko ya kumtoa Rooney kwa kiasi kikubwa yalipelekea Russia kusawazisha goli na kuiongezea presha England kwenye mchezo wao ujao dhidi ya Russia siku ya Alhamisi.
Safu ya ulinzi ya Hodgson ilikuwa imara kwa kiasi kikubwa na kumudu mashambulizi ya kushtukiza kutoka kwa wachezaji wa Russia.
England walicheza vizuri hususan katika kipindi cha kwanza ambapo walikuwa wameujaza uwanja Stade Velodrome huku wachezaji wa Russia wakiwa wanakimbia kutafuta mpira ulipo.
0 comments:
Post a Comment