KLABU ya soka ya Yanga inaendelea na mazoezi yake katika uwanja wa Taifa kujiandaa kuwakabili Mo Bejaia ya Algeria, katika mchezo wa kombe la shirikisho barani Afrika hatua ya Makundi, tayari Yanga imefikisha jumla ya wachezaji 28 katika usajili ulioenda CAF kwa ajili ya michuano hiyo kufuatia kuongezwa kwa wachezaji wa nne Hassan Kessy Ramadhani, Juma Mahadhi, Andrew Vicent 'Dante' na golikipa Beno Kakolanya bado Yanga ina nafasi ya kuongeza wachezaji 2 zaidi ili kutimiza idadi ya wachezaji 30.
Nadir Haroub ataukosa mchezo huo kwa kuwa anatumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyoipata dhidi ya GD Sagrada Esperanca , hata hivyo, Yanga tayari ina mabeki mahiri wa kuweza kuziba nafasi hiyo Vicent Bossou, Kelvin Patrick Yondani, Andrew Vicent , Mbuyu Twite ama Pato Ngonyani.
0 comments:
Post a Comment