Taarifa kutoka vyanzo vya ndani ya klabu ya Simba zinaeleza kuwa, mshambuliaji wa machachari wa Mwadui Jamal Simba Mnyate amemwaga wino kuitumikia klabu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Msimbazi.
Inaelezwa kwamba Mnyate amesaini mkataba wa miaka miwili na amesajiliwa kwa kitita cha shilingi milioni 15.
Ikumbukwe kwamba, Manyate ndiye aliwaua Simba kwa kuifungia timu yake ya Mwadui goli la pekee lililoipa ushindi katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara raundi ya pili uliopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment