Tuesday, June 14, 2016

Vincent Bossou
BEKI wa kati wa Yanga, Mtogo, Vincent Bossou atajiunga na wenzake leo kambini nchini Uturuki. Yanga imeweka kambi katika hotelki ya Rui mjini Antalya, Uturuki kujiandaa na mchezo wa kwanza wa Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Mouloudia Olympique Bejaia Juni 19, mwaka huu, utakaofanyika Uwanja wa Unite Maghrebine mjini Bejaia, Algeria.

Bossou hakuondoka na Yanga Dar es Salaam Alfajiri ya jana kutokana na kuchelewa kurejea nchini baada ya mapumziko kwa sababu ya kile alichoripoti, matatizo ya kifamilia.

Abdul aliyeumia kwenye mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), au Azam Sports Federation Cup (ASFC) Mei 25 mwaka huu Yanga ikishinda 3-1 na akaenda kujitonesha akiichezea timu ya taifa, Taifa Stars ikifungwa 2-0 na Misri Juni 4, mwaka huu.

Kwasababu hiyo, Juma Abdul anatakiwa kuwa nje kwa wiki mbili, hivyo beki mpya, Hassan Kessy anaweza kuanza mapema kuteleza upande wa kulia baada ya kusajiliwa mwezi uliopita kutoka kwa mahasimu, Simba SC.

Mbali na Juma Abdul, wengine walioachwa ni Malimi Busungu, kipa Benedictor Tinocco na mshambuliaji Paul Nonga ambao hawamo kwenye programu ya kocha, wakati kinda Yussuf Mhilu hakwenda kwa sababu jina lake halijasajiliwa Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amesafiri lakini hatacheza mechi hiyo ya kwanza ya Kundi A kwa sababu anatumikia adhabu ya kadi nyekundu, aliyopewa kwenye mchezo uliopita dhidi ya Sagrada Esperanca nchini Angola.

Kiungo Salum Telela ni mchezaji pekee aliyemaliza msimu na Yanga ambaye hajasafiri, kwa sababu hajapewa mkataba mpya baada ya kumaliza wa awali.

Mechi hiyo itachezeshwa na marefa wa Morocco, Bouchaib El Ahrach atakayepuliza kipyenga akisaidiwa na washika vibendera, Redouane Achik na Youssef Mabrouk.

Baada ya mchezo huo, Yanga itarejea Dar es Salaam kuwakaribisha mabingwa wa Afrika, TP Mazembe Juni 28 katika mchezo wake wa pili.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video