Thursday, June 16, 2016

Slaven Bilic akishangilia baada ya Payet kufunga goli dhidi ya Albania jana.
Kocha wa West Ham United Slaven Bilic jana alikuwa kwenye TV akiangalia mchezo kati ya Ufaransa na Albania, akifanya uchambuzi wa mchezo huo ambao mchezaji wake Dimitri Payet alikuwepo dimbani.
Kwa bahati nzuri nyota wake huyo aliifungia Ufaransa goli la pili katika dakika ya 96 baada ya Griezmann kufanya hivyo dakika ya 90.
Dimitri Payet (29) amekuwa kwenye kiwango bora kabisa katika michuano hii na mpaka sasa ana magoli mawili akiwa ni moja ya wanaongooza kwa ufungaji mpaka sasa..
Kocha wake sasa, ambaye bado haamini kama Payet ni kijana wake, alishangilia kwa furaha ya ajabu baada ya Mfaransa huyo kufunga goli na kuwaacha wachambuzi wenzake hoi

Tazama video hapa

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video